ZOEZI LA KUFUKUA MIILI ILIYOFUNIKWA NA KIFUSI CHA GOROFA DAR, YAMALIZIKA HII LEO

Zoezi la kufukua miili iliyofunikwa na kifusi baada ya gengo la gorofa 16 kubomoka siku ya tarehe 29, Machi 2013 katika mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es salaam, imemalizika hii leo huku miili iliyopatika katika kifusi hicho ikifikia watu 34


Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wa mkoa, Mhe. Mecky Sadiki. Sadiki ametoa takimu hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari
 
“ Idadi tuliyo itoa yawatu waliuwawa katika jengo hili ni 34, huku waliookolewa ni watu 18 ambapo kati yao, 14 tayari wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku wengine 4 bado wanapewa matibabu katika hispitali ya taifa Muhimbili” Amesema Sadiki

Hii leo kuna vichwa viwili vya binadamu vimetolewa kwenye kifusi hicho, ambapo Mhe. Mecky Sadiki amesema wanawaachia madaktari kwa uchunguzi zaidi ilikuweza kuwatambua watu hao

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum Suleiman Kova amesema kuwa idadai ya watu wanaoshikiliwa kwa kuhusika na kuanguka kwa jengo hilo imefikia watu tisa baada ya mtu mwingine kukamatwa na kuongezwa katika orodha ya watuhumiwa. Amesema Kamanda Kova


EmoticonEmoticon