MALAWI ACHENI KUTAPATAPA, RUDINI MEZA YA MAZUNGUMZO ASEMA MHE. MEMBE, ATAMBA KUWA NA USHAHIDI KAMA MLIMA KILIMANJARO


SERIKALI ya Tanzania imeitaka Serikali ya Malawi iache kutapatapa katika mgogoro wa mpaka wa Malawi, baada ya Rais wa Malawi Joyce Banda kutangaza kwamba 


serikali ya Tanzania imeweka mtu anayetoa taarifa ya mazungumzo hivyo hawapotayari kuendelea na majadiliano hayo.

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa mambo ya nje ya nchi Mhe. Benard Membe alipokuwa akiongea na wanahabari hii le jijini Dar es salaam, na kusema kuwa malawi inapaswa kurudi kwenye meza ya mazungumzo.

“Hatua ya Malawi itavuruga mazungumzo yetu, sisi tunawaomba waache kutapatapa watulie na waachane na hoja za kupeleka mgogoro huo katika mahakama ya kimataofa ya haki (ICJ) kama ilivyo panga” Alisema Membe

Tanzania kamwe aiogopi hatua ya Malawi ya kuutangazia Ulimwengu kuwa wanamgongano na Tanzania. alisema Membe

" Tunao ushadidi kama mlima Kilimanjaro, wakutosha kumaliza mgogoro huo. Tulichokifanya nikupeleka joo la wataalamu Ujerumani na kwingineko na hata kwenda ICJ tukotayari" alisema Membe

Rais wa Malawi Joyce Banda akiwa na Rais wa Marekani Barack Obama

Aidha Membe amesema, hatua walioichukua Malawi ni kukiuka makubaliano waliojiwekea Novemba 17 mwaka jana hapahapa Jijini Dar es salaa. Hivyo kuitaka Malawi kurejea kwenye meza ya mazungumzo ambapo juhudi za usuluishi wa Kidiplomasia unaendelea.

Malawi inamtuhumu Dr. John Tesha the executive secretary of the forum kwa kutoa siri za mazungumzo hayo hivyo kudai kuwa mgogoro huo auwezi kumalizima kwa njia ya Kidiplomasia.

Hapo awali serikali ya Rais Joyce Banda bila kushauriana na Tanzania ilitoa vibali kwa makampuni mawili ya kigeni kutafuta mafuta katika eneo la ziwa ambalo linamilikiwa na Tanzania.


EmoticonEmoticon