KUTOKA BUNGENI
Hii itakuwa historia tangu Bunge hili kuanza, ambalo ni Bunge la 10 kikao cha13, baada ya Wabunge kuacha hitkadi za chama na kusimamia ukweli na hali alisi juu ya Tatizo la maji nchini
Hii leo Bungeni, Bajeti ya wizara ya
Maji leo haijapitishwa na wabunge, kwakukataa kuunga mkono hoja mpaka njia madhubuti zitakapoletwa kwaajili ya tatizo hilo huku wakilalamika bajeti iliyotengwa ni ndogo kwa jinsi tatizo lilivyo
Wabunge walipaza sauti zao na kumtaka Waziri wa maji na umwagiliaji Mhe. Jumanne Magembe ajipange nakuacha kuwasilisha hotuba yenye nyaraka za uongo kwao
"Wabunge wengi walisikika wakisema, takweimu hizi umetoa wapi, mara hili eneo halipo tanzania umelitoa wali.... nilazima tusimamie ukweli...siungi mkoni hoja" walimalizia
Wabunge hao ambao
walikataa kuunga mkono hoja huku kila mtu akilia na kukosa maji
jimboni mwake wakishangaa hotuba ya waziri ambao imeelezea miradi
mingi iliyotekelezwa
Hatahivyo hoja hiyo
haikupitishwa mpaka itakapo jadiliwa tena bungeni hapo na Mh-Spika wa
Bunge Anne Makinda akalazimika kuahirisha bunge huku akiiagiza
serikali ikae pamoja na kamati ya bajeti kutokana na kuonekana kuwa
bajeti iliyotengwa mwaka huu ni ndogo na haitaweza kumaliza kelele za
maji,hivyo kamati ya bajeti pamoja na serikali zikutane pamoja ili
wajadili pesa hizo watazitoa wapi
Katika kipindi cha
maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri mkuu Bungeni, imebainika kwamba
Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuzalisha mkaa duniani kiasi
ambacho kinatishia mazingira ya nchi yetu
"Waziri alijibu hali hiyo sinjema na isiendelee kwani inahatarisha rasilimali zetu, hivyo kuagiza swala hilo kushugulikiwa"
Tanzania ni moja kati ya nchi 10
zinazozalisha mkaa duniani huku asilimia 3 ya mkaa unaotumika duniani
ukitoka Tanzania ambapo kwa siku Tanzania huzalisha Tani 2650 sawa na
Tani milioni 10 kwa mwaka ,,,na hapo hapo mkaa huliingizia taifa
dola milioni 650 (zaidi ya sh-bilioni moja )vile vile biashara hiyo
inategemewa na familia zaidi ya milioni 1 nchini
EmoticonEmoticon