Wajasiriamali wameshauriwa
kutoogopa kukopa na kutumia taasisi za mikopo katika kuendeleza
biashara zao
Hayo yamesemwa na Gershom
Mpangala ambaye ni Meneja Masoko wa FINCA
(FINCA Tanzania Limited)
alipokuwa akifanya mahojiano na Blog hii. FINCA imekuwa ikitoa mikopo
kwa wajasiriamali zaidi ya Elfu 70 hapa Tanzania
Mpangala amesema, swala la
wajasiriamali wengi kuogopa kukopa ni moja ya kikwazo cha kutoendelea
kwa biashara nyingi.
Aidha amewataka
wajasiriamali kutambua kuwa hata wafanya biashara wakubwa au ambao
wanamiliki biashara tofauti tofauti wamefanikiwa zaidi kwa kutumia
mikopo kwenye biashara zao
“ Wajasiriamali wakubwa,
mfano wanaofungua ma Benk na huduma nyingine kubwa katika jamii wame
fanikiwa kutokana na kukopa, wakope au wahudhurie semina zinazo
fundisha jinsi ya kuendeleza biashara kwakutumia mkopo, watafanikiwa
zaidi” Alisema
Nidhamu
ya Pesa, pia ni msingi wa kuendeleza biashara yako, ujue jinsi gani
ya kupata Faida na kuokoa hela ya mtaji wako... hichi pia ni kikwazo
kwani wengi hutumia faida anayo pata na mtaji bila kujua atumie pesa
hipi katiya hizo ilikuendeleza biashara yake.
Ikiwa
leo ni siku ya wajasiriamali Duniani, kwa Tanzania siku hii imeachwa
kwenye mitandao kwani wajasiriamali wengi hawajui siku hii
EmoticonEmoticon