Mhe. John Nkamia kushoto wakati akiongea na Blog hii: Picha na campasvision.blogspot.com |
Zaidi ya watu Elfu 27 Mkoani Singida
wanaishi kwa kula Mizizi kutokana na ukosefu wa chakula tangu mwezi
wa kumi na mbili mwaka jana, huku Serikali ikilifumbia macho swala
hilo licha ya kuwa na taarifa hizo
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Kondoa
Kusini Mhe. Juma Nkamia alipoongea na Blog hii maeneo ya Bungeni
Jijini Dar es salaam, Nkamia alielezea masikitiko yake kwa serikali
kushindwa kutoa ufumbuzi licha ya kupewa taarifa kwa muda sasa
“Tatizo la wananchi wa singida kukosa
chakula nila muda sasa, tayari nimetoa taarifa kwa Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, Waziri wa Kilimo na Chakula Prof Jumanne Magembe
lakini hakuna hatua yoyote iliyo fanywa kuwa nusuru wananchi na jaa
kali” Alisema Nkamia
Jumla ya watu Elfu 27, kutoka tarafa za
Kwa Mtoro, Farkwa, Goima na Mondo hawana chakula hivi sasa, Alisema
Mbunge huyo na kuongeza kuwa taarifa amefikisha kwa wahusika wakuu
pamoja na kumtaarifu mkurugenzi wa kitengo cha maafa katika ofisi ya
Waziri Mkuu lakini hatua yoyote haijachukuliwa.
Mhe. John Nkamia, ameelezea kuwa
angeweza angetatua tatizo hilo lakini inashindikana kutokana na idadi
ya watu pamoja na mshahara wake hauwezi kutatua tatizo na kulimaliza
kabisa hivyo kuililia Serikali kuokoa wakazi wa maeneo hayo na njaa
hiyo.
Naiomba serikali isisubiri watu
wapoteze maisha ndio waende kutoa msaada, kwani hali hii imetokana na
kutopatikana na chakula cha kutosha katika msimu uliopita hivyo
kuwalazimu wakazi wamaeneo hayo kukubwa na baa la njaa
EmoticonEmoticon