KAMPENI UDSM NI BALAA, WAGOMBEA WANADI SERA ZAO UCHAGUZI KUFANYIKA APRIL 29


Washabiki wa Mkolwe Egidy wakimsindikiza baada ya kushuka jukwaani. Egidy anagombea urais wa DARUSO
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, hii leo wamefungua rasmi kampeni za ugombea nafasi za uongozi wa juu chuo ni hapo

Mwanamke pekee katika kinyang'anyiro hicho Bi. Mashingia Stella
Wagombea hao wapatao wa 5, wa 3 wakigombea nafasi ya Urais huku wawili wakigombea nafasi ya Makamu wa raisi

Blog hii ilifanya mahojiano na Raisi wa DARUSO ambaye anatarajia kumaliza muda wake bwana Bokombe Itembe, ambaye alielezea kuwa kampeni hizo zitakuwa za wiki moja na juma tatu ya wiki ijayo ambayo itakuwa tarehe 29.04.2013

 

“Kampeni zimeanza rasmi leo, wagombea wameanza kunadi sera zao jukwaani kwa muda wa wiki moja kisha jumatatu uchaguzi utafanyika ilikupata viongozi wapya wa DARUSO” alisema Bokombe

Bokombe aliwataka wanafuzni wa chuo hicho kutosusia uchaguzi huo kwani kura zao ndizo zitaleta mabadiliko wanayo yataka, kususia hakuta saidia kitu. Alisema 


Aidha baadhi ya wanafunzi walilalamikia mchakato huo kuwa sio wahaki kwani kuna wagombea ambao walianguka kwenye uchaguzi wa awali lakini bado wameingia kwenye kampeni hizo kama wagombea

“Mtu ameangushwa, baada ya watu 100 kuto mcahgua lakini baadae anakuja kama mgombea nani kamchagua wakati watu 100 tayari walimkataa? Hafai kutuongoza wala hatumtaki” 

wakati mahojiano hayo yakiendelea kelele zilizuka Ndani ya hall ambako kampeni hizo zikifanyiaka kisha umati wawatu ulizuia mahojiano kuendelea kutoakana na kelele nyingi

 

Blog hii iliweza kusikia wanafuzni wakilala mika, wengine wakiendelea kuwa nadi wagombea wao

Hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa baadhi ya wagombea hao wamepandikizwa na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini kwa maslahi yao..kitu ambacho wagombea wote wamekanusha kuwa sikweli

Upinzani mkali kati ya wagombea ulionekana waziwazi kila mtu akielezea jinsi gani atawasaidia na kuwatumikia wanafunzi wa chuo hicho na ukomavu wake katika siasa ya chuo hicho

HABARI PICHA 
thecampasvision.blogspot.com


EmoticonEmoticon