Serikali
imeanza mchakato wa kutekeleza miradi ya ubia kati ya sekta binafsi
na sekta ya umma ilikukuza maendelea katika jamii
Akiongea
kwenye mkutano huo ulifanyika hii leo katika hoteli ya TravelTain
jijini Dar es salaam na kuwahusisha wadau wa sekta binafsi na sekta
ya umma Afisa Biashara wa manispaa ya kinondoni bwana Ananias Jacob
amesema lengo nikukuza maendeleo ya kibiashara katika manispaa ya
kinondoni
“Kikao
iki nichamara ya kwanza, lengo ikiwa ni kuungana na sekta binafsi
katika kukuza maendeleo katika manispaa hii ukizingatia sekta binafsi
ina mchango mkubwa sana kwenye ukuaji wa maendeleo” Alisema Jacob
Aidha,
kwa upande wa wadau wa Sekta binafsi Poul Mashauri kutoka kampuni ya
The bernchmark of excellence (EASB ) amesema wameshukuru serikali
kuwashirikisha katika kukuza uchumi, ikiwa ni pamoja na mambo ya
tehama kati yao na sekta za umma.
“Mkutano
huu unamaana kubwa kwetu kwamba, serikali inatambua mchango wetu
katika kukuza uchumi hasa wa manispaa yetu kwani sekta ya umma
itatupo tupa sapoti mabadiliko lazima yataonekana” alisema Mashauri
Mashauri
aliongeza kuwa, katika mambo yanayo fanyika baina yao na sekta ya
umma kuwepo na taarifa kwa ambazo wanapewa wananchi iliwaweze kujua
juu ya maendeleo yao.
EmoticonEmoticon