BIASHARA ZA MNADA- BUNJU ZIMEPAMBA MOTO, VITU BEI CHEE

Wakazi wa Bunju na viunga vyake Jijini Dar es salaam nje kidogo ya mji, huwa wana ifurahia sana siku ya mnada kwani mnadani pana furika sana kwa watu wakila rika huudhuria siku hiyo.

Wao wakienda Mlimani City au Home Shoping Centre sisi tunakutana hapa kwaajili ya mahitaji muhimu tena kwa bei poa... Masikini kwa masikini tunachangiana, siku ya soko ni Kila alhamisi ya wiki



Pamba zote kali zinapatikana, masista duu wa Bunju tuna tokelezea bila shaka tena hadi 1000 moja unapata Top Kali nguo za watoto usiseme

Kizuri zaidi katika siku hii vitu bei ni chee hivyo wananchi wengi wa Bunju ambao ni wakipato cha chini hupata vitu kwa bei poa kabisa




Pamoja na Neema ya punguzo la Bei linalo wawezesha wakazi zaidi ya Elfu 2000 wanaohudhuria sokoni hapo kumudu lakini Soko la Bunju B halina choo cha kuhudumia watu hao siku ya Mnada 

Serikali ingeweza iangalie utaratibu wa kujenga choo cha kulipia ilikuweza kuhudumia wakazi waeneo hilo na kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko



Kwa vitu vidogovidogo vya kupikia kama ilivyo pichani, kuanzia miambili 200/=  unapata mfuniko, 300 mwiko na Ungo 500 tu, na  mazagazaga kibao kwa wale wanaitaji mambo ya kuzawadia kwenye Kitchen Party hapa si mahali pa kukosa kila Alhamisi 

Pichani ni Josephine Joseph, akifurahia jambo mnadani hapo
 Wale mnao anza maisha msijiuliza marambili Bunju B pana kila kitu kwa ajili yenu usiangaike sana kwani masikini wote tunakutana hapa Shoping ya kufa mtu


Hapa unaweza kupata Dishi zima lenya vyombo kwa Elfu 10,000 tu, endapo ukinunua chombo kimoja kimoja itakugarimu maelfu 10 kibao lakini Mnada wa Bunju mambo ni tofauti


Mnada huo ambao hukaa mara moja kwa wiki inahudumia jumla ya Mitaa Kibao ya Bunju, ambao inakadiriwa kuhudhuriwa na wakazi wa eneo hilo zaidi ya Elfu mbili kwa kila alhamisi 

Wafanya Biashara wa maeneo haya uhama hama kutokana na ratiba za minada ya maeneo haya. Mnada wa Tegeta Kibaoni hukaa kila Ijumaa huku maeneo ya Boko ni kila Jumanee na Bunju nikila Alhamisi pia wanatoa huduma hii mpaka maeneo ya Bagamoyo.


EmoticonEmoticon