Askari wa Jeshi la Polisi wakilivuta gari la Mbunge Huyo juzi eneo la tukio Chuo cha AIA |
Baada
ya Mhe. Godbelss Lema kuhusishwa na vurugu za chuo chauhasibu Arusha
( Arusha Institute of Acountancy), hatimaye akamatwa na Jeshi la
Polisi baada ya kibarua kizito cha kupiga kambi nyumbani kwake usiku
kucha
Habari
zilizo chapishwa na Tovuti ya chama hicho, zinadai kuwa Mbunge huyo
hawezi kukamatwa mpaka pale Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda
atakapotoa kibali cha yeye kukamatwa
Tarifa
ambazo blog hii imefuatilia zina sema kuwa Lema tayari ametiwa
mikononi mwa jeshi la polisi baada ya kukamatwa usiku wa manane
nyumbani kawake ili kujibu tuhuma zinazo mkabili
Siku
mbili zilizo pita Mhe Lema alikuwa kwenye umati wa wanafunzi wa chuo
cha Uhasibu Arusha akiwatuliza hasira wakiwa na lengo la kuandamana
kutokana na kifo cha mwanafunzi mwenzao Henry Koga ambaye aliuwawa
kwa kuchomwa kisu na watu wasio julikana
Mbunge
huyo pia anadaiwa kuchochea maandamano yaliyosababisha vurugu kiasi
cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo kuzomewa na kupopolewa mawe
na wanafunzi wa chuo hicho
Mhe.
Lema alikwenda chuoni hapo ambapo nikaribu kabisa na nyumbani kwake
kwa lengo la kutuliza gasia hizo, kitendo ambacho jeshi la polisi
ilikiita cha uchochezi
VIDEO IKIONYESHA MHE. LEMA AKIONGEA NA WANAFUNZI KATIKA CHUO HICHO
Hatahivyo,
Mhe. Godbless Lema ni miongoni mwa wabunge waliozuiliwa kuingia
Bungeni kwa siku 5 baada ya kuhusishwa na vurugu zilizozuka Bungeni,
Mhe.
Lema alizuiwa kuingia Bungeni kwakosa la kuwakataza askari kumkamata
Mhe Tundu Lissu aliamriwa kutoka nje ya Bunge na Spika wabunge Mhe.
Job Ndungai kwakosa la kuingilia hoja ya Mhe. Mwigulu Nchemba Wabunge
wengine waliozuiwa ni Mhe. Tundu Lisu, Joseph Mbilinyi, Ezekiel Wenje
na Peter Msigwa.
Lema
hivi sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Arusha akiusishwa na
kuchochea vurugu za wanafunzi wa chuo hicho kuandamana, ambapo jeshi
la polisi lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao
MKUU WA MKOA ARUSHA NAYE ALITINGA ENEO LA TUKIO KUTULIZA GASIA , NAHALI YA EWA IKACHAFUKA BAADA YA WANAFUNZI KUMZOMEA
EmoticonEmoticon