UMEME VIJIJINI - NEEMA YAJA, EU KUISAIDIA TANZANIA
Wizara ya Nishati na Madini imekamilisha makubaliano ya fedha za msaada kutoka NORWAY kwaajili ya umeme vijijini, ambayo nikiasi cha Kr 700 ambayo ni karibu USD 140 sawa na Billioni 200 za Kitanzania
Uhakika wa kukamilisha miradi ya umeme kwenye wilaya mpya 13 ambayo itagarimu kiasi cha Billioni 70 hasa vijijni itaenda kwa wakati, Aidha bado maongezi na wafadhili wengine juu ya miradi ya umeme nchini inaendelea huko Brussels.
Viongozi wa juu wa Wizara ya Nishati na Madini hapo jana, walifanya kikao cha majadilianao na EU ilikukamilisha makubaliano ya kukamilisha miradi ya umeme ambapo Mei 3,2013 EU mishion itakuwa Dar ilikufanikisha miradi hiyo
Kikao hicho kilicho mhusisha kaimu Mkurugenzi wa wizara hiyo na Balozi wa EU pamoja na wadau wengine wa sekat hiyo, lengo ni kuondoa tatizo la umeme.
Aidha EU itatoa Grants kwenye miradi ya Transmission, Distribution, Energy, Efficiency, Renewerbale energy pamoja na Capacity building kwa wizara hiyo
EU imeamua kuifanya Tanzania nchi muhimu sana kwa ushirikiano wake na Afrika, hivyo kuamua kukamilisha miradi mbalimbali ya umeme nchini.
Hatahivyo, Bwawa la mtera limeweza kufikisha kiasi cha chini cha uendeshaji wake(Minimum Level) cha 690 M.A.S.I kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.
Taarifa kutoka ndani ya Wizara hiyo zinasema kuwa wanatarajia kiwango hicho kuongezeka ili kuweza kufikia hatua nzuri ya uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo ambalo hivi karibuni lili punguza kiwango chake cha uzalishaji kutokana na kina cha maji kupungua.
EmoticonEmoticon