SERIKALI YASUSIA SIKU YA WATOTO WA MITAANI 12,APRIL


Kutoka Kulian ni, Sophia Temba (KIWOHEDE), Edger Mhando Mgeni rasmi kutoka TCRF,

SIKU ya motto wa mitaani ambayo imeadhimishwa hii leo kote Duniani, Serikali ya Tanzania imeonyesha wazi kutoijali siku hiyo licha ya viongozi kuwa na taarifa na maadhimisho hayo

Katika maadhimisho hayo yaliyofanywa na vituo 5 vya watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu  jijini Dar es salaam, hakukuwa na kiongozi yoyote wala mwakilishi kutoka serikalini licha kupewa mwaliko na kuitambua siku hiyo

Tulipo hoji juu ya kutokuwepo kwa serikali  hasa WIZARA ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Ustawi wa Jamii na Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii pamoja na mamalaka ziingine ambazo zinahusika kwa namna moja amanyingine katika kuangalia watoto nchini

Watoto wanao lelewa na kituo cha KIWOHEDE wakiimba wimbo kwa uchungu 

Blog hii ilifanya mahojiano na Sophia Temba Kutoka KIWOHEDE ambaye anawafundisha watoto kutambua haki zao, ambaye alisema kuwa walituma barua na kuwasilisna na Afisa ustawi wa jamii bwana Darius Damas kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuwa angekuja katika maadhimisho haya

“Afisa Ustawi wa Jamii bwana Darius Damas, ndiye tuliamini angekuja kwani ana barua na anajua juu ya siku hii, pamoja na Wizara zinazo husika kwa ujumla zinatambua juu ya siku hii kwani hii ni siku iliyoanzishwa na umoja wa mataifa, sio hapa tu” Alisema

Sophia Temba, aliiomba serikali ijaribu kupunguza idadi ya watoto waishio mitaani kwani hivi sasa hali inatisha huku mazingira hatarishi na manyanyaso yakiwaandama watoto hao. Alisema

Watoto wanao lelewa na kituo cha Dogodogo Centre Bunju wakiotoa Burudai 

Naye Edgar Muhando, ambaye alikuwa mgeni rasmi kutoka TCRF – Jukwaa la haki za watoto, aliiomba Serikali kukaa pamoja na vya vya kulinda watoto na kuangalia siku hii ilikupiga kelele kwa jamii juu ya kulinda haki za watoto.

Edger amesema, Jamii inatakiwa kujua sio watoto waliovituoni tuu ndio wapewe msaada na wale waishio mitaani waachwe bila msaada, kwani wote wanahaki ya kupata Elimu, Malazi na haki zote za motto. Alisema Edger

Baadhi ya watoto waliohudhuria maadhimisho hayo
Jumla ya watoto 150 kutoka vituo vya KIWOHEDE, DOGODOGO CENTRE, JUKWAA LA WATOTO (TCRF) GNRC na VIJANA FOUDATION FORUM walijumuika katika maadhimisho hayo wakiwa na ujumbe mzito juu ya haki zao hasa watoto ambao wanakaa mitaani

Hivisasa katika jijila Dar es Salaam jumla ya watoton 5800 wako mtaani wakiomba omba na kuzingirwa na maisha yasio kuwa na matumaini ya ustawi wao

Blog hii inaitaka serikali kuonyesha nia yake ya dhati kama kweli wanahuzunishwa na watoto wanao nyanyasika mitaani, kuto hudhuria katika maadhimisho hayo ni kuwazidishia uyatima kwani hakuna anaye onekana kujali juu ya watoto hao

Kaulimbiu ya siku hii ni "Mitaani ndio Nyumbani kwetu" kauli ambayo inatakiwa kupotea kabisa kwani nyumbani hapawezi kuwa ni mitaani kwa kurandaranda


EmoticonEmoticon