Washirika wa jukwaa la wazi la semina
za jinsia na maendeleo GDSS linalo ratibiwa na TGNP, hii leo
wameitaka serikali kurudia uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya katiba
ya wilaya, kata na mitaa
Tamko hilo limekuja baada ya taasisi
hiyo kueleza kuwa mchakato huo uligubikwa na Ubaguzi wa kijinsia,
Rushwa, Udini, na siasa huku miongoni mwa watu 7 watakao wakilisha
mitaa hakuna nafasi ya walemavu
Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa
habari hii leo TGNP, katibu wa GDSS bwana Badi Darusi amesema kuwa
nilazima Serikali kurudia mchakato huo ilimakundi yaliyo achwa
pembezoni kama walemavu na wanahabari wapewe nafasi
“Hakuna anaye wakilisha walemavu,
watu 7 ambao ni wanawake 2 wasichana 2, wanaume 2 na wengine 1 hakuna
mlemavu...walemavu hawana mwakilishi mabaraza ya katiba” alisema
Darus
Darus amesema, katika swala la Siasa
kuchukua nafasi kubwa. Vyama vya siasa vilikuwa zinatumia fursa ya
kufanya kampeni chafu kinyume nataratibu zilizo wekwa na Tume ya
taifa ya mabadiliko ya katiba.
Aidha wameelezea kuwa mchakato huo pia
uligubikwa na vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji uliofanywa na baadhi
ya viongozi wa mitaa na vyama vya siasa hali iliyopelekea kutoa tamko
lao hivyo kuitaka serikali kurudia tena zoezi la uchaguzi wa mabaraza
ya katiba.
EmoticonEmoticon