MTOTO ATOROKA NYUMBANI KWAO KWA KUTESWA

Mtoto wa miaka 12 ametoroka nyumbani kwao na kuja katika vituo vya utangazaji vya ITV akiomba kupelekwa kwa mama yake mzazi baada ya kuchoshwa na manyanyaso ya mama wa kambo pamoja na baba yake

Mtoto huyo Tekla Adolf, ambaye anakaa Makuburi External na anasoma darasa la 6 katika shule ya ATLAS PRIMARY SCHOOL iliyoko External


Tekla amesema miongoni mwa mateso anayo yapata nikipigo kikali kutoka kwa mama yake wa kambo aliye mtaja kwa jina la JANET LYMO kuwa ni kung'atwa kwa meno na mama yake huyo siku zingine anamnyima chakula


Baba wa mtoto huyo anaitwa Benard Adolf, ambaye naye hushirikiana na mkwewe Janet kumtesa mtoto Tekla.

Blog hii ilimpigia mama wa mtoto huyu simu ambaye huko mkoani Tanga nakukiri kufahamu mateso anayo pata mwanaye lakini hushundwa kuchukua hatua kwani baba wa mtoto huyo hayuko tayari kuruhusu yeye kuishi na mtoto huyo.

Blog hii inafatilia zaidi juu ya tukio hilo ikiwa nipamoja na kufikisha taarifa polisi ilitaratibu za kisheria zichukue mkondo wake. habari zaidi zitakujia baadae


EmoticonEmoticon