LULU KUTOSHIRIKI KUMBUKUMBU YA KANUMBA APRIL 12

Lulu akilia baada ya kupewa dhamana 

Wakati ndugu,jamaa, marafiki na wapenzi wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba ambaye anatimiza mwaka mmoja tangu alipofariki dunia April 7. 2012. 

ambapo kumbukumbu yake itafanyika katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es salaam tarehe 12. April mwaka huu, imebainika kwamba Lulu amekatazwa kushiriki sherehe hiyo

Akizungumza na Habarimpya kwa masharti ya kutotajwa jina lake mtandao mmoja wa wanafamilia ya Lulu , amesema kwamba lulu hatashiriki katika sherehe hizo kutokana na sababu za kiusalama

"Nikweli Lulu alimpenda sana Kanumba, na ingawa inaaminika kwamba ndiye aliyekuwa chanzo cha kifo chake, ila kama binadamu angependa kushiriki mazishi yake, napengine kuiaga mwili wake kwa mara ya mwisho, ila ilishindikana kwa sababu alikuwa lumande"kilisema chanzo chetu na kuongeza.

"Kipindi Kanumba anazikwa Lulu alikuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi wa kesi yake, na hivi sasa mazishi hayo yameandaliwa tena kwa maana ya sherehe za kumbukumbu yake, Lulu bado angependa kuungana na ndugu,jamaa,marafiki na mashabiki wa Kanumba,lakini kutoka na suala la usalama wake hatuwezi kumruhusu ashiriki".

Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anatuhumiwa kwa kosa la kuuwa bila kukusudia msani mwenzake ambaye pia alikuwa mchumbake, siku ya April 7 mwaka jana,baada ya kudaiwa kumsukuma na kujigonga ukutani wakati walipokuwa katika ugomvi wa mapenzi.


EmoticonEmoticon