Kenya imepata Raisi Mpya wa
awamu ya Uhuru Kenyatta pamoja na Makamu wa Rais ambaye ni Willium
Ruto, ambao wamechukua nafasi ya Rais Mwai Kibaki alie acha uongozi
hii leo. Uhuru ameapishwa chini ya katiba ya nchi hiyo katika uwanja
wa Moi Kasarani jijini Nairobi,
Wageni mashuhuri
walihudhuria katika sherehe hizo, nipamoja na Rais wa Tanzania Mhe.
Jakaya Kikwete na First Lady mama Salma Kikwete, Edward Lowasa na
wengineo.Yoweri Kaguta Museven wa Uganda, Rais wa Sudan Kusini Salva
kiir mayardit. Hatahivyo, Yoweri Museven ndiye aliye toa hotuba kwa
niaba ya Wageni wote waalikwa kwenye sherehe hizo
Aidha Kenyatta ndiye rais
mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuongoza nchi ya Kenya akiwa anaumri
wa miaka 51 na ni mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya Hayati Jomo
Kenyatta. Hata hii leo aliapa kwa kutumia Biblia aliyotumia baba yake
Mpinzani mkuu wa Uhuru
Kenyatta, Raila Odinga ambaye naye ni mtoto wa waziri mkuu wa kwanza
wa nchi hiyo, hakuweza kuhudhuria sherehe hizo nayuko nchi AFRIKA
KUSINI kwa mapumziko
Kenyatta na naibu wake
William Ruto wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu katika
mahakama ya uhalifu wa kivita ICC . Wanadaiwa kuwa washukiwa wakuu wa
ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika miaka mwaka 2007.
Aliye kuwa mpinzania wake bwana Raila Odinga hakuhudhuria sherehe hizo na badala yake yuko nchini Afrika ya Kusini akila bata
EmoticonEmoticon