NAULI MPYA ZA MABASI NA DALADALA BALAAA, SUMATRA WABARIKI

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Ahmad Kilima alitangaza

Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. 

1. Nauli za Daladala – Jiji la Dar es Salaam

Umbali wa Njia
Kiwango Kipya cha Nauli
Mfano wa Njia
Kilomita kati ya 0 – 10 (Na mipaka ya Jiji Kati)
Sh 400/=
Ubungo – Kivukoni
Kilomita kati ya 11 – 15
Sh 450/=
Mwenge – Temeke
Kilomita kati ya 16 – 20
Sh 500/=
Tabata Chang’ombe – Kivukoni
Kilomita kati ya 21 – 25
Sh 600/=
Pugu Kajiungeni – Kariakoo
Kilomita kati ya 26 – 30
Sh 750/=
Kibamba – Kariakoo

2. Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu

Daraja la Basi
Nauli ya zamani kwa km-abiria
Nauli mpya kwa km-abiria
Mfano wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia


Basi la Kawaida kwa njia ya lami
Sh 30.67
Sh 36.89
DSM–Mbeya Km 833
Sh 30,700
Basi la Kawaida kwa njia ya vumbi
Sh 37.72
Sh 46.11
S/wanga-KigomaKm 551
Sh 25,400
Basi la hadhi ya kati (Semi Luxury
Sh 45.53
Sh 53.22
DSM–Mwanza Km 1,154
Sh 61,400








Mabasi ya masafa marefu yaendayo mikoani
Nauli za usafiri wa mabasi makubwa ya masafa marefu nauli hizo zimeongezeka kwa viwango tofauti. Mathalani. Basi la kawaida kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ni Sh30,700, njia ya vumbi kutoka Kigoma hadi Sumbawanga Sh25,400 na basi la hadhi ya kati (Semi Luxury) kati ya Dar na Mwanza ni Sh61,400, wakati basi la hadhi ya juu (Luxury) kati ya Dar na Arusha ni Sh 36,000.Kilima alisema: 

“Kuanzia Aprili 12 mwaka huu, kati ya kilometa 0 hadi 10, nauli ya daladala itakuwa Sh400 badala ya Sh300 zinazolipwa hivi sasa.“Pia nauli za mabasi ya kwenda mikoani zimeongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, mabasi ya kati kwa asilimia 16.9 na mabasi ya daraja la juu kwa asilimia 13.2,” alisema.

Kilima alisema nauli za - Mabasi ya mikoani zimepanda kutoka Sh30.67 hadi Sh36.89 kwa kilometa - Mabasi ya daraja la kawaida katika njia za lami. Kwa upande wa - Mabasi ya kawaida kwa njia ya vumbi imepanda kutoka Sh37.72 hadi Sh 46.11 kwa kilometa na kwamba - Mabasi ya hadhi ya kati, nauli zimepanda kutoka Sh45.53 hadi Sh 53.22 kwa kilometa.- Mabasi ya hadhi ya juu nauli zimepanda kutoka Sh51.64 hadi Sh58.47 kwa kilometa.Kupanda kwa nauli kunatakiwa kwenda sambamba na huduma bora na kwamba Sumatra imepiga marufuku kutumia wapigadebe kuuza tiketi za safari”alisema.

Usafiri wa ReliKatika uamuzi huo, usafiri wa reli pia umepanda ambapo daraja la kwanza Dar es Salaam hadi Morogoro, nauli mpya na ya zamani katika mabano ni Sh21,100, (Sh16,852), Dar hadi Dodoma Sh34,700, (Sh27,788), Dar es Salaam-Tabora Sh54,800, (Sh43,859).Dar es Salaam-Isaka Sh62,100, (Sh49,662), Dar- Shinyanga Sh65,300 (Sh52,229) Dar –Mwanza Sh74,800 (Sh 59,818), Dar- Kigoma Sh75,700, (Sh60,599)

Daraja la pili, 
Dar es Salaam-Morogoro Sh16,600, (Sh13,280), Dar es Salaam-Dodoma Sh26,400 (Sh 21,092), Dar es Salaam-Tabora Sh40,500 (Sh 32,364), Dar es Salaam-Isaka Sh45,800, (Sh36,605), Dar es Salaam-Shinyanga Sh48,000 (Sh38,390),Dar es Salaam- Mwanza Sh54,700 (Sh43,747), Dar es Salaam-Kigoma Sh55,400 (Sh44,305).

Daraja la tatu, 
Dar es Salaam-Morogoro Sh8,800 (Sh6,138), Dar es Salaam-Dodoma Sh13,500 (Sh9,374), Dar es Salaam-Tabora 20,400 (Sh14,173), Dar es Salaam-Isaka Sh22,800 (Sh15,847), Dar es Salaam –Shinyanga Sh24,000 (Sh16,628), Dar es Salaam-Mwanza Sh27,200 (Sh18,860), Dar es Salaam- Kigoma Sh27,500 (Sh19,084).

Akizungumzia tozo za majini, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mamlaka hiyo imeridhia ongezeko la tozo la asilimia 34.3 kwa vyombo vinavyotumia bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Alisema awali TPA walipendekeza tozo hizo kuongezeka kati ya asilimia saba hadi 400 kulingana na aina ya huduma zinazotolewa kwa meli zinazotumia bandari za mamlaka hiyo.


EmoticonEmoticon