Mashine ya hydraform kuzalisha matofali ya bei rahisi |
Wanafunzi 35 kutoka chuo cha Fundi
Stadi (VETA) wamechaguliwa kuendesha mashine ya Hydroform inayo
fyatua matofali ya bei rahisi yatakayo tumiwa na shirika la nyumba la
Taifa (NHC) katika ujenzi wa nyumba zaidi ya Elfu 5000 nchini
wanafunzi 35 watakao hudhuria mafunzo hayo |
Akiongea katika makubalianao na VETA
yautoaji mafunzo kwa wanafunzi hao, Mkurugenzi mkuu wa NHC bwana
Nehemia Kyando Mchechu amesema shirika hilo liko kwenye utekelezaji
wa ujenzi wa nyumba Elfu 5000 za garama nafuu
“ MASHINE ya Hydroform itazalisha
tofali nyingi kwa garama ndogo, pia aiharibu mazingira. Tutakamilisha
ujenzi wa nyumba 5000 ambazo tutaziuza kwa garama za chini hivyo kila
mtu ataweza kununua ”Alisema
Mkurugenzi mkuu wa NHC na Mkurugenzi mkuu wa VETA wakisaini makubaliano hayo |
Mchechu amesema , NHC imejenga nyumba
za Garama ya Millioni 35 tu lakini hizi sasa wanaitaji kupunguza
garama hiyo, japo kuwa bei ya ujenzi wa nyumba inatofautiana mikoa
hadi mkoa kulingana na upatikanaji wa maitaji ya ujenzi
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha VETA
bwana Zebedia Moshi amesema. Chuo hicho kimeanzisha mikakati ya
kuwapatia ajira wanafunzi wanao soma chuo ni hapo ilikukabiliana na
uhaba wa soko la ajira nchini kwani lengo lao nikufikisha asilimia
95% yawanafunzi wanao pata ajira ndani ya miaka 5
“ Ndai ya miaka 5 tunataka vijana
wapate ajira kwa kiwango cha asilimia 95%, kwani hivi sasa ni
asilimia 66% yawanafunzi wanaojiajiri kutoka vyuo vya VETA kote
nchini huku Asilimia 43% wanahajiriwa, kwakushirikiana na wadau
tutaongeza kiwango kilichopo hivi sasa” Aliseam
Jumla ya wanafunzi 35 ambao
wamechaguliwa na NHC watapewa mafunzo ya wiki mbili baadae
watagawanywa kwenye mikoa mbalimbali nchini ikiwemo GEITA,
KIGOMA,SONGEA ,KATAVI TANGA na Dar es Salaam (Kigamboni)
EmoticonEmoticon