Serikali ya Tanzania
imesema itahakikisha kwamba hakuna mtanzania ambaye atakufa kwa njaa
mwaka huu licha ya kuripotiwa kwa baadhi ya maeneo yaliokumbwa na
ukame na njaa kali
hayo yamesemwa na
Waziri wa Uvuvi na maendeleo ya Mifugo Mhe. David Mathayo David hii
leo jijini Da es Salaam, alipokuwa akifanya ufunguzi wa mradi wa
uwezeshaji wakulima na wafugaji vijijini
Waziri Mathayo amesema,
japo kuwa kuna uhaba wa chakula katika baadhi ya maeneo lakini
serikali haita acha kuwafikishia chakula watu hao, na kuwa serikali
inatambua maeneo ambayo yanasumbuliwa na njaa
Waziri Mathayo
amezitaka taasisi binafsi kushirikiana na serikali ma maafisa ugani
ili kuweza kufikia kilele cha mafanikio katika sekta ya kilimo na
ufugaji.
Katika mradi huo kiasi
cha Dola millioni 13.2 zimetolewa na UN ambayo ni sawa na Shilingi
Billioni 20 za kitanzania ili kuwafanikisha wajasiliamali
wadogowadogo kuendesha biashara zao pamoja na kutafuta masoko
kwaajili ya bidhaa zao
Zaidi ya asilimia 75 ya
watanzania wameajiriwa na kilimo, hivyo mradi huu utaleta maendeleo
kwa watanzania kujiendeleza kiuchumi
EmoticonEmoticon