HAPA KAZI TUU.... JOHN POMBE MAGUFULI AANZA NA WIZARA YA FEDHA

HAPA KAZI TUU.... JOHN POMBE MAGUFULI AANZA NA WIZARA YA FEDHA


Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli hii leo amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya fedha na kukuta baadhi ya watendaji katika Wizara hiyo wakiwa hapo ofisini Ikiwa bado ni muda wakazi.

Katika hali isiyoyakawaida, Rais Magufuli pia alitembea kwa miguu akitokea Ikulu kwenda ofisini hapo akiambatana na walinzi wake ambapo alikuta maofisa hao wakiwa awapo kazini.



Watanzania mbalimbali wametoa maoni kwa njia ya mitandao ya kijaa  juu ya ziara hiyo ya kushtukiza kuwa ya kuimarisha uchapakazi kwani viongozi wengi wa serikali wamekuwa wakifanya kazi kimazoea jambo ambalo linapelekea maendeleo kurudi nyuma.

Hivyo kumtaka Mhe Rais JP kuhakikisha kuwa anafanya ziara za mara kwa mara ili aweze kuwawajibisha wafanyakazi wazembe serikalini.

JANET MBENE WASHUKURU WANANCHI WA JIMBO LA SONGWE KWA KUMPA KURA ZA KISHINDO


 MBUNGE mteule katika Jimbo la Ileje mkoani Songwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene (CCM) amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na  Dkt. Jonh
Magufuli anayewania urais.

Akizungumza na wakazi wa Ileje, Mbene alisema ushindi wa kura 27,583 aliopewa na wana Ileje dhidi ya Emmanuel Mbuba wa NCCR Mageuzi aliyepata kura 14,578

atahakikisha anawapa wananchi hao kupitia ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali
zinazowakalibi.

“Awali ya yote niwashukuru wana Ileje kwa kuonesha imani kubwa kwangu, madiwani na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Jonh Magufuli. Wana Ileje wametupa kura za kishindo nami ninawahaidi sitawaangusha katika utekelezaji wa ahadi nilizozitoa kwenu wakati wa kampeni,” 
alisema Mbene.

Kategori

Kategori