Thursday, July 7, 2016

WASHINDI WA FAIDIKA NA AMANA BANK WAKABIDHIWA ZAWADI ZAOKATIKA kuadhimisha kilele cha kampeni ya faidika na amana bank, benki hiyo imewazawadia wateja wake waliobahatika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na kujiwekea akiba zao  katika benki ya amana ambapo makabidhiano hayo yamefanyika leo Jijini Dare s salaam kwenye maonesho ya viwanja vya sabasaba ndani ya banda la benki hiyo.
Kampeni hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti binafsi kujiwekea akiba katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi laki tano na kundelea kwa muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi za vifaa vya matumizi a nyumbani kama luninga, jokofu na nyinginezo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi hizo mkurugenzi wa benki ya amana Dokta Muhsin Masoud amesema kuwa zawadi zilizotolewa leo kwa wateja zimegharimu kiai cha shilingi milioni tano na kuongeza kuwa benki itaendelea kuwafikia wateja wake kila siku na kuwapatia watanzania wote huduma bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na mahitaji yao ili kuwapa faida iliyohalali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.

Nao baadhi ya washindi waliojishindia zawadi wameipongeza benki ya amana kwa kuw karibu na wateja wake na kuiomba iendelee kuonesha ushirikiano huo mzuri kwa watumiaji wote wa benki hiyo.

Monday, July 4, 2016

TANZANIA KINARA KWA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU DUNIANI


Nchi ya  Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa mataifa yanayoshamiri  kwa biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwa ajili ya utumwa wa ngono duniani.

Hayo yamelezwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya kuzuia na kupambana na biashara haramu ya bianadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Bw. Separatus Fella alipokuwa akiongea katika mkutano uliondaliwa na shirka la kimataifa la msaada wa sheria (NOLA) kwa lengo la kutoa elimu juu ya mdahara ya kusafirisha watoto.

"Tanzania ni kusudio,mkondo na chanzo cha usafirishaji wa wanawake na watoto wanaopelekwa kwenye biashara ya utumwa wa ngono katika mataifa mengine, na hii ni kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa nchini Marekani"

Bw. Fella amesema wasafirishaji binadamu wamekuwa wakitumia Tanzania kama chanzo cha kupitisha na kupata watoto wanawake wakufanya biashara hiyo na kuwa serikali itaandaa takwimu za watu walioathirika na usafirishaji huo.

WAZIRI WA ELIMU ATAKA VETA KUUNGANA NA COSTECH


WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako amesema kwa mwaka huu wa fedha, wamejipanga kuhakikisha wanafufua karakana zilizopo na kuhakikisha zinaendana na matakwa ya serikali ya Viwanda.

Akizungumza wakati alipotembelea katika banda la VETA, Ndalichako alisema pamoja na kufufua karakana zilizopo Veta pia wataongeza wigo wa kuhakikisha zinakuwa nyingi na kuboreshwa.

Alisema kazi inayofanywa na VETA ni kubwa ila tatizo lipo kwenye kujitangaza ili kuweza kuuza bidhaa zao.
"Kazi wanayofanya Veta ni kubwa, lakini changamoto ipo kwenye kujitangaza, bado hawajajitangaza katika kutoa huduma zao. Hivyo tutashirikiana na Costech ili kuendeleza VETA na kupunguza kuagiza vitu kutoka nje ya Nchi," alisema.

Ndalichako alisema tatizo linalosababisha la Veta kuwa chache ni gharama zake kwani jengo moja linagharimu bil. 9, hivyo wameshawaagiza Veta kupitia upya gharama kwa viwango tofauti tofauti ili kupata Veta nyingi.

TECHNO YAJA NA SMARTPHONE YA CAMON 9, WATEJA 100 WA MWANZO WAZIGOMBANIA

 Kampuni ya simu ya Tecno yazindua Smartphone ya Camon 9 nchini Tanzania 

• Ina kamera yenye uwezo wa mega pixel 13 

•Yaja na  ofa ya GB 10 kutoka kampuni ya simu ya Vodacom kwa muda wa mwezi moja.


Meneja wa mauzo wa TECHNO Bw Fred Kadilana akielezea ubora wa CAMON c9


Wednesday, May 4, 2016

ASILIMIA 80 YA WATOTO HUPOTEZA MAISHA KWA SARATANI YA JICHO NCHINI TANZANIA
Asilimia 80  ya watoto wenye umri kati ya mwaka 1 hadi 5 wanaougua saratani ya jicho nchini Tanzania hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kuchelewa kupata matibabu ya ugonjwa huo..


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Daktari bingwa wa saratani kutoka hosptali ya taifa Muhimbili Dr. Anna Sanyiwa amesema, bado jamii na wauguzi wa afya ngazi ya mkoa na zahanati awana ufahamu juu ya ugonjwa huo suala ambalo linapeleka waathirika wa ugonjwa huo kuchelewa kupata matibabu na baadae kuwa na upofu au kupoteza maisha..

"Takribani watoto 150 kwa mwaka hupatikana na tatizo hili, asilimia 70 hadi 80 kati yao hupoteza maisha kwa kuchelewa kupata uduma kutokana na uelewa mdogo wa ugonjwa huo" amesema Dr. Sanyiwa

Saratani ya jicho  hutokea kwenye macho yote mawili au kijo moja, ambapo dalili za awali za ugonjwa huo nikuwepo kwa weupe kwenye mboni ya jicho na kwamba ni rahisi kwa familia moja kuwa na watoto wenye ugonjwa huo kwani saratani ya jicho ni miongoni mwa magonjwa yanayo tokana na hitilafu kwenye vinasaba..

Friday, November 6, 2015

HAPA KAZI TUU.... JOHN POMBE MAGUFULI AANZA NA WIZARA YA FEDHA


Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli hii leo amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya fedha na kukuta baadhi ya watendaji katika Wizara hiyo wakiwa hapo ofisini Ikiwa bado ni muda wakazi.

Katika hali isiyoyakawaida, Rais Magufuli pia alitembea kwa miguu akitokea Ikulu kwenda ofisini hapo akiambatana na walinzi wake ambapo alikuta maofisa hao wakiwa awapo kazini.


video

Watanzania mbalimbali wametoa maoni kwa njia ya mitandao ya kijaa  juu ya ziara hiyo ya kushtukiza kuwa ya kuimarisha uchapakazi kwani viongozi wengi wa serikali wamekuwa wakifanya kazi kimazoea jambo ambalo linapelekea maendeleo kurudi nyuma.

Hivyo kumtaka Mhe Rais JP kuhakikisha kuwa anafanya ziara za mara kwa mara ili aweze kuwawajibisha wafanyakazi wazembe serikalini.