MATOKEO MAPYA MWOKOZI WA WAHITIMU 2012, BILLIONI 152 NAZO ZATOLEWA KUKUZA KINGEREZA MASHULENI

Matokeo mapya ya kidato cha nne 2012 yanayotarajiwa kutangazwa siku za hivi karibuni yatakuwa na unafuu zaidi kuliko yale yaliyofutwa ambayo wanafunzi wengi wamefeli


Akiongea na waandishi wa habari ika matokeo hayohii leo jijini Dar es salaam Waziri wa Elimu na Mfunzo ya ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa amesema matokeo hayo mapya yataleta mwanga mzuri wa masomo kwa wanafunzi waliopata maksi za chini na kwamba hakutakuwa na uchakachuaji katika zoezi hilo

“Hakuta kuwa na uchakachuaji, Baraza la mitihani wanafanya kazi kitaalamu… wanafunzi wawe na matumaini ya kuendelea mbele, hakuna anaye penda haya lengo la Serikali nikutaka kuona sekta ya Elimu inasonga na kwa matokeo haya mapya mabadiliko yatakuwepo” alisema Mhe. Kawambwa

Kama ambavyo kamati iliyoundwa kuchunguza matokeo haya na mapendekezo yake imeshauri juu ya kurudia mfumo wa zamani na kutoa nafasi kwa wadau wa elimu kufanya mchakato wa kutoa elimu na maandlizi juu ya mfumo huu mpya itatekelezwa. Alisema Mhe. Kawambwa

Aidha, Wizara ya Elimu imepokea Pound Millioni 60 sawa na Shilingi Billioni 152, Millioni 309 na Laki 400000 ilikukuza ubora wa Elimu katika somo la Kingereza katika shule za Sekondari na za msingi

Kiasi hicho cha pesa kimetolewa na British Council na kitanufaisha Vyuo 34 vya Ualimu, Wakufunzi wa vyuo Laki na zaidi pamoja na wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari nchini




EmoticonEmoticon