Matokeo mapya yaliyo subiriwa kwa hamu
sana hatimaye yametoka hii leo, huku kiwango cha waliofaulu
kikiongezeka na kuwa asilimia 43 hivi sasa kutoka asilimia 9.55 kwa
yale matokeo ya kwanza yaliyo tangazwa tarehe 18 februari mwaka huu.
Jumla ya watahiniwa Laki 397, 138
wamefaulu, wasichana wakiwa ni Elfu 60,751 na wavulana wakiwa ni Elfu
98,858 ikiwa ni jumla ya watahiniwa wa shule Laki 159,609.
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja
waliyopata watahiniwa, inaonyesha kuwa jumla ya watahiniwa Elfu
35,349 wamefaulu katika daraja I – III ambapo kati yao wasichana ni
Elfu 10,924 na wavulana ni Elfu 24,425 ambao hawa ndio wataweza
kujiunga na kidato cha sita mwaka huu kutoka idadi ya wanafunzi Elfu
35,349 ambao walifaulu hapo awali na kuacha idadi kubwa ya wanafunzi
Waliofaulu kwa daraja la IV ni wavulana
ni Elfu 74,433, wasichana ni Elfu 49,827 ambao kwa ujumla wanafikia
Laki 124,260 sawa na asilimia 33.54, Walipata sifuri kwa sasa ni Laki
210,846 sawa na asilimia 56.92. Matokeo ya wali jumla ya wanafunzi
Laki 210, 846 walipata sifuri ambao ni sawa na silimia 56.92
Akitangaza matokeo hayo hii leo jijini
Dar es salaam, Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Shukuru
kawambwa amesema maandalizi ya matokeo yaliyo tangazwa sasa
yamechakatwa kwa utaratibu wa Fixed Grade Ranges lakini yakafanyiwa
standalization.
“Matokeo yaliyofutwa yalikuwa
yamechakatwa kwa kutumia utaratibu wa fixed grade ranges utaratibu
uliotumika kwa matokeo haya mapya lakini kwa hawamu hii tumefanya
standalization ilikuweza kupata matokeo haya kama ambavyo tume maalum
ilivyo pendekeza” alisema
Dr, Kawambwa alielezea Fixed Grade
Ranges kuwa hutumia viwango vya aina moja kuchakata matokeo kwa
masomo yote bila kujali kiwango cha kufaulu kwa somo husika, viwango
hivyo hubadilika kila mwaka kulingana na ufaulu wa watahiniwa kwa
kila somo husika
Aidha, katika mfumo wa Fixed Grade
Ranges viwango vya aina moja hutumika kuchakata matokeo kwa masomo
yote bila kujali kiwango cha ufaulu kwa somo husika. Viwango vya
kuchakata matokeo hutumika hivyo hivyo kila mwaka bila mabadiliko .
Alisema Dr. Kawambwa
kuanzia sasa na kuendelea baraza la
mitihani litaandaa matokeo ya kidato cha nne na sita kwa kutumia
mfumo wa fixed grade ranges na standardisation. Alisema waziri
KUANGALIA MATOKEO MAPYA KIDATO CHA NNE INGIA HAPA
KUANGALIA MATOKEO MAPYA KIDATO CHA NNE INGIA HAPA
EmoticonEmoticon