MALENGO YA MILENIA 2015 KUTOTIMIA BILA MAJI KUWAFIKIA WANANCHI KWA MASAA 24 NCHINI

Swala la uharibifu wa mazingira umetajwa kuwa chanzo cha kukauka kwa vyanzo vya maji nchini, na kuchangia kwa tatizo la uhaba wa maji



Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa maji na Umwagiliaji Prof. Jumanne Maghembe alipokuwa akifungua mkutano wa wiki moja wa kujadili tatizo la maji kwa nchi za Afrika ambapo amewataka watanzania kutunza vyanzo vya maji




“Watu wengi huaribu vyanzo vya maji katika maeneo yanayo wavunguka hii pia ni changamoto kwetu, matumizi ya mkaa na kuni ndio huchangia”

Prof. Jumanne alisema kuwa hivi sasa mchakato wa kufikisha maji kwa vijiji 682 nchi nzima umeanza, hivyo kufikia mwaka 2015 mradi huo wakufikisha maji utakamilika.




Mkutano huo unalenga kuahinisha njia za kupunguza upotevu wa maji kabla ya kumfikia mteja ili kufanikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa ukanda wa Afrika ifikapo mwaka 2015

“Watu Millioni 65 barani Afrika wana uhitaji mkubwa wa maji, huku nchini Tanzania ni Asilimia 63 ya watu wanahitaji maji. Hivyo wadau wa maji wanaangalia ni njia gani za kuwafikia watu hawa “Alisema Prof. Jumanne Magembe



Hatahivyo, Dawasa kupitia mpango wake maalum wa kuboresha maji katika jiji la Dar es salaam imepanga kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita Millioni 300 hadi Lita Millioni 756 kwa siku



Dawasa pia imedhamiria kuongeza idadi ya waliounganishiwa maji kutoka kaya 110,000 kwa sasa mpaka 590,000, ambapo huduma ya maji itakuwa kwa masaa 24 tofauti na hivi sasa maji hupatikana kwa masaa 8 tu.

Katika hatua mbalimbali za kuwafikishia wananchi maji kwa asilimia kubwa nimoja ya malengo ya millenia kwa mwaka 2015, ambapo mapato ya Dawasa yatafikia Shilingi Bilioni 9 kwa mwezi tofauti na ilivyo sasa, wana kusanya shilingi bilioni 3 tu kwa mwezi


EmoticonEmoticon