Jukwaa la Katiba Tanzania
limeamua kwenda mahakamani kupinga mwenendo wa uundwaji wa katiba mpya kwa
madai kuwa mchakato unaotumika siyo wa kidemokrasia.
Akiongea na Wana habari leo
Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bw. Deus Kibamba amesema kuwa,
Tume ya katiba inapeleka mchakato kwa haraka hivyo kuwanyima fursa wananchi
kutoa maoni yao na kwamba wanaiomba mahakama
kusitisha zoezi la kukusanya maoni.
“Tumeamua kwenda mahakamani kutafuta haki ya
watanzania, kwani tumejaribu kufanya kila jitihada na kutoa matamko lakini
hayakuzaa matunda hivyo Mahakama itatusaidia kuleta haki” Amesema Kibamba
Kibamba amesema, Tumejaribu
kutoa tarifa kwa ngazi za Kibunge kwa kuonana na spika, kuonana na waziri wa
sheria na katiba pamoja na kujaribu kwa ngazi za juu kwa kuomba kukutana na
rais lakini haya yote hayaja zaa matunda hivyo tunaenda mahakani ambako haki ya
watanzania inapatikana huko.
Bwana Kibamba aliendelea
kusema, Tume ya katiba imeshindwa kutekeleza misingi 5 ya uundwaji wa katiba
hivyo kuwanyima wananchi fursa ya kuleta mabadiliko kikatiba.
“Mwenendo wa mchakato wa
katiba mpya hauto zaa katiba mpya Tanzania, nasema hivi kwakuwa wananchi
hawajui kitu kabisa mchakato unaharakishwa bila hamasa yoyote hii haraka
niyanini.” Alisema
Alitaja misingi hiyo 5 kuwa
ni, Ushirikishwaji wawana siasa, kutokuwepo kwa mahakama ya kikatiba nchini
kiasi kwamba wanalazimika kwenda mahaka zilizopo kufikisha madai yao. Tayari
jukwaa hilo limeandaa mawakili 10 kusimamia kesi hiyo wakiongozwa na Rugemeleza
Nshulla.
Aidha Bwana Kibamba ameongeza
kuwa, Mchakato wa katiba mpya si vyema kuendeshwa kisiasa hivyo Wabunge
wasihusishwe katika mchakato huo na kuwa wananchi wapewe nafasi kubwa ya kutoa
maoni yao ili kuepusha msukumo wa chama kimoja.
Katika hatua nyingine Jukwaa
la katiba limeitaka Tume ya katiba kueleza wananchi ni lini watatoa rasimu ya
katiba kwani muda waliotoa tayari umepita na kwamba Mabilioni wanayotengewa na
serikali yanaenda wapi.
Wakati huohuo, Jukwaa la katiba
limemtakaWaziri wa Mambo ya ndani Dr. Emanuel Nchimbi asikiuke katiba ya
jamuhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 19, kwani wizara yake imepanga
kukiuka ibara hiyo,
Dr. Nchimbi akisoma bajeti ya
wizara yake mapema Bungeni amesema serikali inapanga kupeleka muswada Bungeni wakuzuia
mihadhara na maandamano yote nchini kwani wanaofanya hivyo wanasababisha
uvunjifu wa amani
“Kuzuia mihadhara ndio itakuwa
kama kuchohea kwani kila mtu anahaki ya kusema na kutoa maoni yake” alisema
Kibamba.
EmoticonEmoticon