Wafanyabiashara ambao hawatatoa risiti pindi wauzapo bidhaa zao watatozwa
faini ya shilingi Millioni 3, ikiwa pamoja na wale watakao nunua bidhaa bila kudai risiti kutozwa Milioni 1 kwa kosa hilo
Hayo
yamesemwa na Bi. Alvera K. Ndabagaye ambaye ni Afisa Elimu mwandamizi
wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) alipokuwa akitoa mafunzo kwa
wafanya biashara wa vifaa vya ujenzi na vipuri vya magari katika
manispaa ya Kinondoni ya jinsi ya kutumia kifaa kipya cha kielctronic
kwaajili ya kukatia risiti
“ Nihaki
ya kisheria kudai risiti, pia nikosa kisheria kutotoa risiti baada ya
kuuza bidhaa, faini kwa asiye toa ni Millioni 3 na kwa yule asiye dai
ni Millioni 1” alisema Bi. Alvera
Aidha
Bi. Alivera amewataka Watanzania kutambua kwamba utozwaji wa kodi
ndio pato la taifa hivyo kuwa mstari wa mbele kudhibiti upotevu wa
kodi, nakuacha kulalamika pale ambapo wanakosa huduma za jamii kwani
kodi ndio hukamilisha hayo yote
“Tunalalamika
serikali isipo kamilisha huduma za kijamii lakini hatujui kuwa kodi
zetu ndio hufanya haya yote.. tuwe wazalendo tuzuie mianya ya kupotea
kwa kodi ilikuleta maendeleo”
Kwamuda
sasa TRA ikokwenye zoezi la kutoa Elimu kwa wafanyabiashara wa ngazi
mbalimbali nchini ya jinsi ya kutumia mashine ya kielectroniki
kwaajili ya kutolea risiti wakati wa mauzo ya bidhaa zao
Hatahivyo
kifaa hicho hakitakuwa na ongezeko la kodi iliyopo sasa bali
itashugulikia utoaji wa risiti tu.
EmoticonEmoticon