WAJASIRIAMALI WAPEWA MBINU ZA KUKUZA MITAJI YAO

 



WAJASIRIAMALI KOTE NCHINI WAME TAKIWA KUTUMIA MBINU ZA KITEKNOLOJIA KUKUZA MITAJI NA BIASHARA ZAO ILIKUWEZA KUKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA NCHINI

HAYO YAMESEMWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM NA WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA MHE. MAKAME MBARAWA WAKATI AKIFUNGUA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI ZAIDI YA 150 KUTOKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

MAFUNZO HAYO, YATATOA FURSA KWA WAJASIRIAMALI NCHINI KUTAFUTA SOKO LA NDANI NA NJE YA NCHI, PAMOJA NA KUTATUA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA IKIWA PAMOJA NA KUKUZA MITAJI YAO

TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA WANAOHITIMU VYUO VIKUU NI CHANGAMOTO KUBWA, MBINU ZA UJASIRIAMALI ITASAIDIA KUKABILIAANA NA TATIZO LA AJIRA, KWANI WATAJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

MHE. MBARAWA ALISEMA, MBINU WANAZO FUNDISHWA  ZITASAIDIA KUKUZA MITAJI YAO PAMOJA NA KUWASAIDIA KATIKA MIKOPO KUPITIA BENKI YA DUNIA

AIDHA MKURUGENZI MKUU WA TUME YA SAYANSI NA TEKNOLOGIA DR. HASSAN MSHINDA, AMESEMA KUWA MAFUNZO HAYA YANALENGA KUKUZA BIASHARA KWA NJIA YA TEKNOHAMA ILIKUWEZA KUKABILIANA NA HITAJI LA MASOKO LILILOPO HIZI SASA

MASOKO YAPO, LAKINI MBINU ZA KITEKNOLOGIA BADO AZITUMIKI IPASAVYO KUWAWEZESHA KUKUZA BIASHARA ZAO MPAKA NJE YA NCHI”

MAFUNZO HAYO YATAFANYIKA KWA SIKU MBILI HAPA JIJINI DAR ES SALAAM, CHINI YA TUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA COSTECH, KWA USHIRIKIANO NA WATU WA MAREKANI, PAMOJA NA TAASISI MBALIMBALI ZA KIBIASHARA.

JUMLA YA WAJASIRIAMALI 150 KUTOKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WAMEHUDHURIA MAFUNZO HAYO.


EmoticonEmoticon