Akiongea
na waandishi wa habari jijini Da es salaam, Mweyekiti wa chama cha
Wauguzi mkoani Da es salaam, Bi Joan Bigirwa amesema chama hicho
kinahitaji mwanasheria ilikubaini kosa likowapi pindi muuguzi
anapoangukia mikononi mwa sheria
“Wauguzi
wengi wana huhukumiwa na kila mtu pale kosa linapotokea kama kufariki
mgonjwa akiwa hospitali na kulaumiwa kuwa ni uzembe wao bila
kuangalika kama hakukuwa na vitenda kazi au ni kosa la Daktari,
lakini jamii yote ulaumu Wauguzi” Alisema
Hali
hiyo imepelekea dhamira ya kuweka wanasheria ilikusaidia wauguzi
pindi kunapotokea makosa kwani tupo kwaajili ya kutetea wauguzi
pamoja na haki ya wagonjwa ya kupata huduma. Alisema Bi. Joan
Hatua
hiyo imetangazwa ikiwa ni siku chache kuelekea siku ya wauguzi
Duniani ambapo kitaifa siku hiyo itahadhimishwa mkoani Lindi
Naye,
Bi. Wilielmina Niwabigira ambaye ni Afisa Muuguzi (DUCE) na
mwenyekiti wa Tanzania Nursers Association (TANNA) amesema kuwa
mishahara midogo, wagonjwa wengi kuliko idadi ya wauguzi, mazingira
yakazi yasiyo rafiki ya kazi husababisha wauguzi wengi kuonekana
hawafanyi kazi ipasavyo na kutojali wagonjwa
“Hakuna
vitendea kazi, wagonjwa ni wengi kuliko idadi ya wagonjwa pamoja na mishahara kidogo husababisha wauguzi tuonekane kama hatujali wagonjwa
kitu ambacho sio kweli” alisema Bi. Niwabigira
Kama
huduma zikiboreshwa na kuwepo kwa vitendea kazi vya kutosha kulingana
na idadi ya wagonjwa tunao wahudumia, whakutakuwa na malalamiko kwa
wateja juu ya huduma zetu lakini kuna muda tunashindwa kulingana na
mazingira yasiyo rafiki kwetu tuwapo kazini
“Mgonjwa
anaweza kuja hospitali dakika za mwisho lakini akifariki hulaumu
wauguzi, kumbe angewahi hayoyote yasinge tokea. Kuna muda wagonjwa
nao waelewe hilo”Alisema
Hatahivyo
chama hicho kimeeleza kuwa hakuna Hospitali hata moja nchini ilikidhi
vigezo vya kuweka wauguzi wa kutosha kama ambavyo sheria ua Huduma za
Afya inasema, kwani mpaka sasa idadi ya wagonjwa ni huwa kubwa kuliko
ya wauguzi na madaktari
Kaulimbiu
ya maadhimisho ya wauguzi kitaifa kwa mwaka 2013 inasema kutekeleza
mpango wa millenium ifikapo 2015. ambapo wanalenga kupunguza vifo vya
watoto chini ya miaka mitano, kuboresha afya ya mama, kudhibiti
maambukizi ya virusi vya ukimwi, malaria na magonjwa mengine ya
kuambukiza kam kifua kikuu
EmoticonEmoticon