Kutokana
na swala la ukosefu wa Ajira nchini, Baraza la uwezeshaji wananchi
kiuchumi NEEC limeamua kuwapa elimu ya kujiajiri vijana 40 ambao ni
wahitimu wa vyuo vikuu ili kuendeleza biashara zao na kuajiri
wengine.
Akiongea
hii leo katika kituo cha Ujasiriamali cha chuo kikuu cha Dar es
salaam UDSM, Katibu mtendaji wa Baraza hilo bwana Anecleti Kashuliza
amesema wameamua kutoa elimu hiyo ili kuweza kutoa ajira kwa kundi
kubwa la vijana kwa lengo la kupata ajira na kisha kuajiri wengine
“Njia
ya kukabiliana na tatizo la ajira nikuwapa elimu ya mitaji pamoja na
kuenedeleza biashara zao, ambapo vijana 40 tuliowapata baada ya
mchujo watasaidiwa kukuza biashara zao” Alisema
Vijana
wengi wa kitanzania hawana ujuzi wa biashara wa vitendo, kwani
wamezoeya njia ya nadharia zaidi kuliko vitendo hivyo kushindwa
kujiajiri hata pindi wanapo hitimu masomo yao. Alisema Bwana
Kashuliza
Hatapindi
vijana wanapo jaribu kujiajiri, ukosefu wa kuendeleza mitaji
huwaangusha, pia ujuzi wa kinachohitajika sokoni pia nimdogo
“Uwezo
wa biashara ya kushirikiana (Net-Working) inawashinda vijana
waliohitimu vyuoni kuweza kufanikisha kujiajiri wenyewe, hivyo
tutawawezesha vijana hawa kujiajiri ikiwa pamoja na kukuza mitaji yao
iliwaweze kuajiri na wengine” Alisema
zaidi
ya vijana Laki 8 ambao huingia katika soko la ajira kila mwaka
nchini, laki wakiwa ni wahitimu wa vyuo vikuu, vijana Elfu 4 tu kati
yao ndio huajiriwa kila mwaka hapa nchini, hii umaanisha kwamba idadi
ya vijana Laki 7 na 60 Elfu hujikuta bila ajira.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon