SERIKALI YATAKIWA KUWAKUMBUKA WAFANYA KAZI WA MAJUMBANI




Serikali imetakiwa kutekeleza mkataba wa kimataifa wa shirika la kazi Duniani ILO mbayo iliahidi huko Geneva mwaka 2011, ili kutekeleza maslahi ya wafanyakazi wa majumbani, ambapo Tanzania ni nchi ya Pili kwa kuwa na wafanyakazi wengi wa majumbani barani Afrika.

Mwaka 2011 tarehe 15 June huko Geneva, siku moja kabla ya kupitisha mkataba wa kimataifa wa shirika la kazi sheria no 189, Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania DR. Jakaya Kikwete aliahidi kutekeleza mkataba huo na kuuridhia, hivyo serikali imeombwa kutekeleza ahadi hiyo.

Akiongea katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka barani Afrika na kufunguliwa na Waziri wa Kazi na ajira nchini Mhe. Gaudencia Kabaka , Mratibu wa mtandao wa wafanyakazi wa majumbani kanda ya Afika Bi. Vicky Kanyoka amesema wengi wa waafanyakazi wa majumbani wanakumbwa na changa moto nyingi hivyo kuitaka serikali kushugulikia changamoto hizo

“Serikali nyingi za Afrika zilipigia kura kutaka kuwepo kwa mkataba wa kimataifa ambao utatetea maslahi ya wafanyakazi wa majumbani, Tanzania ikiwepo lakini ni nchi chache sana zimeanza kutekeleza yale yaliyo takiwa kushugulikiwa” Alisema

Afrika inajumla ya vyama 19 vya kutetea maslahi ya wafanya kazi, lakini tuliafikiana kushugulikia haki ya kupewa ajira, muda wa kazi, mikataba, kima cha mishahara na jinsi ya kuwaendeleza kielemu wafanyakazi wa majumbani. Alisema Kanyoka

Naye Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanya kazi Zanzibar bwana Khamis Mwinyi Mohamed, amesema kuwa wana jitahidi kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa majumbani na kutaja haki zinazotakiwa kufuatwa juu ya wafanyakazi hao.

“Tuli pendekeza mishahara ya wafanyakazi wa majumbani kiwe Elfu 60 kwa Zanzibar na Elfu 65 kwa Tanzania bara mpaka sasa hakuna anaye tekeleza haya, nasisi bado tunajitahidi kuhakikisha kuwa tunatekeleza” Alisema Mohamed

Aidha Tanzania ina jumla ya wafanyakazi wa majumbani Zaidi ya milioni moja huku wengi wao wakiwa ni wanawake. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kazi Duniani Tanzania ni nchi ya Pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hao kwa asilimia 80.5, ikiongozwa na Mali yenye asilimia 86.8.

Nchi zilizo fanikiwa kufanikiwa katika kushugulikia tatizo hili kikamilifu ni nchi ya Afrika Kusini na Mouritius.

Mkutano huo wa siku tatu, ambao umeanza hii leo May 29 mpaka 30, unafanyika jijini Dar es salaam, umeshirikisha jumla ya wawakilishi 75 kutoka nchi za barabi Afrika, vyama mbalimbali vya kutetea maslahi ya wafanyakazi.


EmoticonEmoticon