Vurugu kati ya Jeshi la Polisi na baadhi ya wakazi wa Mtwara
zinaendelea hivi sasa, ambapo Mahakama, Kituo cha Jeshi la Polisi na Taraja
pamoja na nyumba ya Mbunge vimeharibiwa kutokana na maandamano vurugu hizo,
maeneo yaliyo adhirika zaidi ni Mtwara mjini na Mkindani
Maandamano hayo yametokana na kupinga Bajeti
ya Wizara ya Nishati na Madini ambayo imewasilishwa hii leo Bungeni
Habari zilizo ifikia Blog hii zinasema kuwa
mpaka sasa, Maafa yanaendelea katika mkoa huo huku mabomu na risasi zikirindima
kila kona watu wakikimbia hovyo huku polisi nao wakijitahidi kutuliza gasia
hizo
Daraja la mkindani limevunjwa, mahakama ya mwanzo ya Mitenga
imechomwa moto, kituo cha polisi, pamoja na maeneo ambapo kuna makapuni ya
kuchimba gesi navyo vimechomwa moto.
Tayari mtu mmoja amekufa, huku wengine wakihofiwa kufa kutokana na ali hiyo. Nyumba ya Mbunge na ya mtangazaji
wa TBC nayo imechomwa moto katika vurugu hizo
Habari zaidi zinasema kuwa Gari ya JWTZ nalo imepata ajali
ikiwa njiani kuelekea Mwara ikitokea Nachingwea, na msaada wa kitabibu
unahitajika kwa Askari hao
Hatahivyo, Waziri wa nishati namadini Mhe. Sospetre Muhongo
amesema serikali imeendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Lindi na Mtwara kujua
faida ya jinsi watakavyo faidika na Gesi hiyo pia ameeleza kuwa wakazi wa
mtwara waachane na fujo na maandamano kwani sio njia sahihi ya kutatua mgogoro
huo
Naye Waziri wa madini kivuli ambaye Mwakilishi wa kambi ya
Upinzani Mhe. John Mnyika ameitaka serikali kuweka wazi mikataba yote ya madini
ilikuondoa migogoro miongoni mwa wananchi
EmoticonEmoticon