Tanzania imeanza
kutekeleza kiwango cha kimataifa cha uzalishaji kitakacho tekelezwa
na viwanda pamoja na makampuni mbalimbali nchini kwa lengo la
kunufaisha jamii
Kiwango hicho kilicho
tolewa na shirika la viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na
Shirika la viwango la kimataifa (ISO) linalenga makampuni kuzalisha
bidhaa kulingana na kiwango cha jamii inayo izunguka na bila kuadhiri
mazigira
Akiongea na Waaandishi wa
Habari hii leo katika uzindushi wa kiwango hicho mapema leo jijini
Dar es salaa, Mkurugenzi wa TBS bwana Leandri S. Kinabo amesema
kiwango hicho kitatumika na nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki
na Tanzania ndio walipewa nafasi ya kuandaa kiwango hicho
“Kiwango kimezinduliwa
Tanzania lakini kitatumika na nchi zote za Ukanda wa Afrika mashariki
kwa maana Kenya, Uganda watatumia kiwango hichi” Alisema Bwana
Kinabo
Kinabo aliongeza kuwa,
Lengo la kiwango hicho nikuzitaka kampuni na viwanda vinavyo zalisha
bidhaa katika ukanda huu kuzalisha bidhaa zao huku zilikila mazingira
na rasilimali watu katika maeneo yanayo wazunguka hatimaye kunufaisha
jamii hiyo
“Makampuni yatatakiwa
kutosababisha maafa, kulinda mazingira, rasilimali watu pamoja na
njia ambazo zitaleta maendeleo katika eneo husika kama
barabar”alisema
Naye mwakilishi wa Katibu
mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ambaye ni bwana Odilo Majengo
amesema kuwa kiwango hicho kinajulikana kama TZS 1323 ndicho
kitatumika kwa makampuni yote ukanda wa Afrika Mahsriki kwa ajili ya
viwanda na makampuni.
EmoticonEmoticon