Wananchi wametakiwa kutoa ushahidi kwa wale wanao wauzia damu ilikuweza kusaidia katika kudhibiti tatizo hilo
Akiongea na Blog hii, Muhamasishaji
jamii upatikanaji wa damu salama Bi. Hadija Juma kutoka shirika la
Msalaba Mwekundu (READ CROSS) amesema watu wengi hutoa malalamiko juu
ya kuuziwa damu lakini hawako tayari kutoa ushahidi juu ya madai yao
ilikuwezesha kudhibiti tatizo hilo
Wafanyakazi wa Read Cross wakitoa huduma ya kwanza kwa msichana aliye poteza fahamu muda mfupi baada ya kutoa damu
Hali hiyo aina madhara kiafya kwa mujibu wa Bi. Hadija Juma
“ Changamoto kubwa kwetu ni swala la
kuuzwa kwa damu, watu wengi wanalalamika lakini tunapo jaribu kufanya
utafiti hawako tayari kusema zaidi hivyo tunashindwa kudhibitisha,
hali ambayo inapelekea kudhibiti uuzwaji damu kuwa mgumu” Alisema
Aidha, amewahasa wanawake kwa wanaume
kujitolea kila mara katika kuchangia damu, kwani uhitaji wa damu ni
mkubwa katika jamii. Alisema kwa wanaume unafaa kutoa Damu mara 4 kwa
mwaka ambayo nikila baada ya miezi 3 huku kwa wanawake ni mara tatu
kwamwaka ambayo ni kila baada ya mwiezi mi nne
“Kidaktari Wanaume inatakiwa
kuchangia damu mara 4 kwa mwaka, huku wanawake ni mara 3 kwa mwaka”
alisema
Naye Katibu wa shirika hilo Bi. Grace
Mtui Mawalla amesema kuwa shirika hilo lina hadhimisha miaka 150
tangu kuanza kwa huduma zake za uokoaji kwa jamii Duniani, ambapo
kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika mkaoni Arusha
“Maandhimisho haya yanafanyika
Duniani kote, kitaifa yanafanyika mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi
atakuwani mkuu wa mkoa huo Bwana. Magesa Murongo, kauli mbiu yeti ni
Miaka 150 ya huduma za kibinadamu” Alisema
Jumla ya Vijana 289 wa shirika la
msalaba mwekundu wamejitokeza kuchangia damu katika makao makuu ya
shirika hilo, kati ya hao vijana 61 ndio wametoa damu, 27 wameshindwa
kutokana na matatizo ya kiafya ikiwemo Presha, huku wengine
wakishindwa kutokana na mambo mbalimbali
Siku hiyo ya maadhimisho ndiyo siku
ambayo muasisi wa shirika hilo Henry Dunant Gustave Maynier alizaliwa
mnamo 8/5/1828 huko Geneva – Uswiss, ambayo nisiku ya Read Cross
Duniani.
EmoticonEmoticon