KINANA, CCM WANAPANGA NJAMA ZA KUMVUA LISSU UBUNGE MAHAKAMANI



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali njama za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana kufufua kesi ya uchaguzi dhidi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa amedai kwamba CHADEMA imekamata nyaraka zinazoonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Kinana amewaelekeza waliowakuwa mawakili wa makada wa CCM waliomfungulia Mh. Lissu kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki mwaka 2010 wafungue rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma iliyotupilia mbali kesi ya makada hao wa CCM dhidi ya Lissu. Kesi ya Mahakama Kuu ilitupiliwa mbali tarehe 27 Aprili mwaka jana.

Dr. Slaa alisema kwamba lengo la njama za Kinana na CCM ni kuhakikisha kwamba Mh. Lissu anafutiwa Ubunge ili asiweze kushiriki katika mchakato wa Katiba Mpya kama mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba litakalojadili na kupitisha rasimu ya Katiba Mpya baadaye mwaka huu. Dr. Slaa alisema: “Kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge, Mheshimiwa Lissu amekuwa mwiba mkali kwa CCM na Serikali yake ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI HABARI HII


EmoticonEmoticon