WANAFUNZI WETU HAWANA UWEZO, KUTOA MAKSI UPYA AITAFICHA UKWELI

Bwana Rakesh Rajani, mkuu wa TWAWEZA 

Taasisi ya TWAWEZA inayojihusisha na tafiti za masuala mbalimbali ya kijamii nchini imeitaka serikali kishugulikia masuala ya msingi yanayoirudisha nyuma sekta ya Elimu nchini

Akiongea na mwandishi wa Blog hii katika ofisi za taasisi hiyo mapema leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bwana Rakesh Rajani ambaye pia alikuwa miongoni mwa wajumbe wa tume iliyoundwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda, kuchunguza chanzo cha matokeo mabaya ya kidato cha nne 2002

Bwana Rakesh amesema matokeo mapya yaliyotangazwa hayana nafuu yoyote bali serikali ishugulikie masuala muhimu yanayoirudisha myuma sekta ya elimu

Nasikitishwa sana na matokeo kufutwa na kutolewa upya, ukweli ni kwamba wanafunzi wetu hawana uwezo wa kieleimu, nibora tungefanya mkakati wa kuwafundisha upya ilikuweza kuongeza uwezo wao nasio kuwapa maksi ili ionekane wanauwezo” Amesema

Rakesh alisema kuwa ingekuwa bora kama tungetoa fursa kwa wale wanafunzi waliofeli kupewa elimu ya kuongeza uwezo wao kupitia vyuo mbalimbali hata kwa mwaka mmoja lakini sio kuwapa maksi tu bila kuongeza ufahamu wao katika elimu.

Karne ya 21 nilazima mwanafunzi apate alama A au B, hii inamaana kwamba anajua kupambanua na kuelewa mambo katika wakati huu, kuwa chini ya hapo inamaana hawezi kupambana na changamoto za karne hii” Amesema

Matokeo ya kidato cha IV na ya kidato cha VI yako chini sana na hayaridhishi, nashangaa watu wamesifu sana matokeo ya kidato cha VI je wamelinganisha ufaulu wa nchi zetu na nchi zinazotuzunguka wakajua sisi elimu yetu inaendawapi kama tunakuwa au tunazidi kupotea

Nchi zinazotuzunguka ufaulu wao ni asilimia 50 sisi bado tuna asilimia 35 nabado tunafanya vibaya nandio maana nikasema nimesikitishwa na matokeo mapya kwakuwa siyo suluhisho la kufeli” Amesema

Aidha akiongelea juu ya majibu mapendekezo ya Tume iliyoundwa na kuchunguza kufeli huko, amesema ni kweli Elimu ya Tanzania inahitaji sera ambayo itakuwa mwongozo wa mfumo wa elimi lakini katika mapendekezo hayo wasisahau Dawa ya sera itakayo fanya mwalimu awena motisha katika kazi yake

Sera yetu isiegemee majengo ya shule tu, vitabu na kusahau motisha kwa walimu kwani wengi wao wamekata tamaa hawana hari ya kazi yao, sera yetu izingatie mambo muhimu sana ambayo yatainua elimu yetu”Amesema Rakesh

Akizungumzia sababu za yeye kutoendelea kufanya kazi na tume hiyo, Bw, Rakesh amesema kipindi cha wiki sita alichopewa na waziri mkuu wakati wa uteuzi wake kilimalizika tangu April 15 mwaka huu na hakuwa tayari kuendelea na ujumbe wa tume hiyo kutokana na majukumu mengine aliyonayo.

Matokeo mapya ya kidato cha nne yaliyotangazwa wiki iliyopita yanaonesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 9 ikilinganishwa na yale yaliyofutwa, wakati huo huo tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza chanzo cha matokeo mabaya inatarajia kukamilisha kazi yake June 15 mwaka huu.


EmoticonEmoticon