NCHI
32 pamoja na makampuni ya ndani 1620 yatashiriki katika maonyesho ya
37 ya biashara ya kimataifa yajulikanayo kama sabasaba yanayofanyika
kila mwaka jijini Dar es salaam, katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia tarehe 28 june mpaka tarehe 8 julai mwaka huu.
Akiongea
na wanahabari katika viwanja hivyo, Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya
maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jackline Malekwe amesema maonyesho
ya mwaka huu yana mabadiliko mengi tofauti na miaka iliyopita.
Katika mwaka huu kutakuwa na mabanda ya Nchi na bidhaa zake huku Tanzania ikiwa na Bandalake ambalo litakuwa na bidhaa za Tanzania (Made in Tanzania) kwa lengo la kuinua biashara ya vitu vinavyo zalishwa hapa nchini. Alisema Bi Jackline
Aidha Bi Jackline amesema mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imepewa wajibu wa kuhakikisha wanakuza wajasiriamali wote nchini na kutoa fursa za biadhaa zao ili kukuza uchumi, na kwamba fursa ya Sabasaba kwa wajasiriamali nikujifunza na kuiga yale watakayo ona wengine wanafanya ilikukuza ufanisi wao
Tayari Maandalizi yame kamilika kwa baadhi ya Mabanda katika viwanja hivyo, ambapo kibanda cha HOME SHOPPING CENTER tayari kilisha pendeza sana na maandalizi yamekamilika
Wakati huo huo Watanzania wametakiwa kuhudhuria maonyesho hayo kwa nia ya kujifunza mambo mbalimbali na siyo kutembea bila ya kujifunza chochote, amesema Bi. Fatma Washoto ambaye ni Meneja masoko wa Home Shopping Centre.
Katika maonyesho haya kutakuwa na utaratibu mpya wa kukata tiketi kutumia mashine, hivyo mtu anaweza kwenda katika maeneo kama Steers - Mkabala na Makumbusho, Mlimani City na katika viwanja hivyo, hii nikutokana na kuondoa usumbufu Getini .
Bi. Jackline alisema kuwa tayari Tiketi za kujiunga na maonyesho ya mwaka ujao 2014 zinatolewa na mamlaka hiyo.
EmoticonEmoticon