TAMASHA LA FILAMU NCHINI KUANZA JULAI MOSI 2013 MKOANI MWANZA

Tamasha la Filamu nchini lijulikanalo kama Tanzania Open Film linatarajia kufanyika katika jiji la Mwanza kuanzia Julai mosi mpaka Julai 7 mwaka huu





Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake Muigizaji Jacob Steven maarufu kama JB amesema hiyo ni nasafi kubwa sana kwa wasanii kwa sababu watapata fursa ya kuonana na mashabiki wao na kuzungumza nao moja kwa moja,


Pia watatumia nafasi hiyo kugawa vyandarua katika Hospitali ya sekoture iliyopo jijini Mwanza ilikuweza kuwasaidia akina mama na watoto katika hospitali hiyo


Meneja wa Habari na mawasiliano wa TBL Edith Mushi amesema, katika miaka miwili iliyopita tangu tamasha hilo kuanza wamejifunza vitu vingi sana kikubwa nikuwa watanzania wengi wanazipenda na kuzikubali Filamu za kitanzania

Aidha Edith, amesema wanaendelea kushirikiana na Sophia Records kuandaa tamasha hilo, Ambapo Mkurugenzi wa kampuni ya Sophia Records bwana Mussa Kissoky amesema waliamua kuanzisha tamasha hilo baada ya kuona kiu ya watanzania kupata fursa ya kukutana na wasanii wao


Hatahivyo, ilifahamika kuwa kutokana na hali yakuwa na vurugu za hapa na pale Tamashahili lilitakiwa kuwa mkoani humo na badala yake likapelekwa mkoani Mwanza



EmoticonEmoticon