Wakati Tanzania ikiungana na nchi zote duniani katika maadhimisho ya kupiga vita Dawa za kulevya. kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Dodoma
Taifa bado lina kabiliwa na changamoto kubwa ya kudhibiti matumizi ya dawa hizo kutokana na wimbi kubwa la vijana kuendelea kujiingiza katika matumizi ya madawa hayo, hali ambayo inatikisa mustakabali wa mendeleo ya taifa
Matumizi ya madawa haya yana ambatana na matukio ya uhalifu, uzururzji na maambukizi ya virusi vya ukimwi ambavyo vinaongezeka siku hadi siku
Akiongea katika maadhimisho hayo, Waziri wa nchi ofisi waziri mkuu sera na uratibu wa Bunge Mhe. Wilium Lukuvi kwa niaba ya Waziri mkuu Mhe. Mizengo Pinda amesema matumizi ya dawa za kulevya ni janga kwa taifa kutokana na vijana wengi hasa walioko shuleni
"Hali hii inatishia mustakabali wa taifa, vijana wengi walioko mashuleni wanazidi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa hizo" Alisema Lukuvi
Aidha Mhe. Lukuzi amesema Vita didhi ya matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya inahitaji ushirikiano wa hali ya juu kwa Watanzania wote kwani Tayari imeshaanza kulichafua jina la Tanzania katika nchi mbalimbali Duniani
Hatahivyo Tume ya Kuratibu udhibiti wa dawa za kulevya kupitia Kamishna wake Bwana Christopher Sekiondo amesema, tume hiyo inakabiliwa na chanagamoto kubwa katika kutekeleza majukumu yake kutokana na biashara ya dawa za kulevya kuhusisha watu wengi wakiwemo wenye nyadhifa za juu na matajiri
" Biashara ya madawa ya kulevya ningumu kutokana na kuwahusisha watu wengi wakiwemo wenye nyadhifa za juu na matajiri" Alisema Bwana Sekiondo
Siku ya kupinga vita ya dawa za kulevya Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 26 mwezi juni ambapo Tanzania iliungana na mataifa mengine katika kukemea Madawa hayo
Tangu mwaka 1999 maadhimisho hayo hufanyika Duniani, huku kaulimbiu ya mwaka huu ikiwa ni FURAHIA AFYA YAKO NA SIYO MADAWA YA KULEVYA

EmoticonEmoticon