Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo
Pinda amewakabidhi rungu Jeshi la Polisi ilikupiga raia ambao watajikusanya au
kuandamana bila kibali cha Jeshi hilo
Akijibu maswali ya papo ka hapoambayo huyajibu kila Alhamisi
Bungeni, Waziri mkuu huyo amesema Polisi wapige tu raia wakati akijibu swali
lililo ulizwa na Mbunge wa Kilwa Mhe. Murtaza Mangungu aliye taka kujua
serikali inachukua hatua gani kwa Polisi wanao piga raia
Mhe. Pinda alijibu kuwa,
“Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye hiki na ukafanya fujo
na ukakaidi ukafanya fujo utapigwa tuu, hakuna
maana nyingine, nilazima tukubaliane kuwa nchi hii ina endeshwa na misingi ya
kisheria sasa kama wewe umekaidi hutaki
unaona kama nijeuri na zaidi wewe ndio jeuri zaidi utapigwa tuu na mimi nasema
wapigeni tuu maana hatuna namna nyingie” alisema kwa msisitizo waziri huyo
Waziri mkuu aliongeza kuwa, Mara ya mwisho hapa Bungeni
nilisema nataka kurudisha hali ya amani na nilisema nilazima turudishe amani
sasa tuache tusiwakamate wakati wanavunja amanani, nyiye wenyewe mtasema
tunawaachai” Alisema
Aidha Kauli hiyo ya Waziri iliyosindikizwa na makofi ya
Wabunge… ilikuwa tofauti kwa Mbunge wa Konde Mhe. Khatibu Saidi Hadji aliyetaka
Waziri huyo kujibu ni kwanini amevunja katiba ya jamuhuri ya muungano wa
Tanzania ibara ya 13 kifungu cha 6-B na 6-E
Kifungo hichi kinasema kuwa, NIMARUFUKU KWA MTU YEYOTE
ALIYESHATAKIWA KWA KOSA LA JINAI KUTENDEWA KAMA MTU MWENYE KOSA HILO, NI
MARUFUKU KWA MTU YEYOTE KUTESWA, KUADHIBIWA KINYAMA AU KUPEWA ADHABU
ZINAZOTWEZA UTU NA KUMDHALILISHA jambo ambalo Waziri alijibu kama ifuatavyo
Waziri mkuu alijibu kuwa, Lazima uweke tofauti kwa mtu aliye
kamatwa na mtu ambaye anavunja sheria, kama wewe umeambiwa usiende kufanya
maandamano ukaenda nilazima tufanye hivyo, na nilazima utii sheria bila
shuruti. Alisema Mhe Pinda
Kwa muda sasa kumekuwa na taarifa hasa maeneo kunakotokea
maandamano na vurugu, Raia kulalamikia polisi kuwa piga hata kuwa teas… ambapo
Waziri mkuu kawakabidhi rungu kuwapiga raia
EmoticonEmoticon