WABUNGE 4 WA CHADEMA NA WANANCHI 60 NA MIKONONI MWA POLISI, MHE MBOWE, TUNDU LISU HAWAJULIKANI WALIPO




Jeshi la polisi  mkoani Arusha limewakamata wabunge 4 wa chadema ambao majina yao hayajajulikana mara moja, pamoja na wananchi wengine wapatao 60 huku msemaji wa kambi rasmi ya upinzani Mhe. Freeman Mbow pamoja na Mbunge wa Singida mjini Mhe. Tundu Lisu wakiwa hawajulikani walipo baada ya polisi kutawanya wafuasi wa chama hicho

Wanachama hao walijikusanya katika uwanja wa Soweto mkoani humo wakiwaaga wale waliouwawa na Bomu hapo Juzi ambapo Polisi ilidai kuwa ni kukusanyika eneo la soweto bila kibali cha sertikali

Kwa habari ambayo Blog hii imeipata kutoka kwa shuhuda huko Arusha nikuwa hali bado ni tete na kuwa kuna majeruhi kadhaa wamekimbizwa katika Hospitali ya mount Meru kwa matibabu zaidi juu ya tukio hilo

Utapata Updates kadri tutakavyokuwa tunazipata 


EmoticonEmoticon