UJENZI WA BARABARA WA WAONDOA MACHINGA ENEO LA MANZESE

Wafanya biashara wadogo kandokando ya barabara ya Morogoro eneo la Manzese jijini Dar es salaam wameendelea kutolewa kwa nguvu chini ya ulinzi mkali wa Polisi na wanamgambo ilikupisha ujenzi wa barabara hiyo


Blog hii ili mtafuta mkuu wa Wilaya wa Kinondoni bwaba Jordan Rwegimbana nakueleza kuwa, wafanyabiashara hao wanaondolewa kupisha ujenzi wa barabara hiyo kwani mkandarasi anaye jenga barabara hiyo alilalamikia kuwepo kwao katika eneo hilo kuwa unakwamisha ujenzi wa barabara hiyo

 "Wilaya ya Kinondoni inamasoko 30, hivyo wafanyabiashara wangeenda huko kufanya biashara mahali ambapo pako sahihi kisheria"Alisema Rwegimbana



Swala la kuwepo uvumi kuwa zoezi la kuwaondoa wafanya biashara hao kunatokana na ujio wa Rais Barack Obama wa marekani, bwana Rwegimbana alikanusha kuwa jambo hilo haliwezekani kwani nimuda sasa wamekuwa wakishugulikia swala la kuwaondoa wafanyabiashara hao katika eneo hilo

 

Kutokana na madai ya wafanyabiashara kulaumu kupotelewa mali zao Bwana Rwegimbana amewataka wafanyabiashara hao kuripoti kwake mara moja ilihatua ziweze kuchukuliwa


Barabara hiyo inajengwa tokea Ubungo mpaka Posta, ikiwani ya ujenzi wa magari ya endayo kasi nchini


EmoticonEmoticon