WATOTO WAOMBA SIKU YAO KUJADILI RASIMU, LHRC NAO WAZIDI KUJITOSA KUTETEA HAKI ZAO



Kituo cha sheria na haki za binadamu, hii leo kimefanya maadhimisho yake ya siku ya mtoto wa Afrika katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam wakiwa na kaulimbiu isemayo Kupinga tamaduni na mienendo hasi dhidi ya watoto ni wajibu wa jamii nzima

Akionge na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Bi Helen Kijo Bisimba amesema kuwa, pamoja na kuwa wameshiriki katika mchakato wa kuhimiza haki za watoto katika katiba mpya lakini wamefurahi kuwa watoto wengi sasa wanauelewa juu ya siku hiyo pamoja na haki zao.

“ Watoto wengi sasa wanaelewa umuhimu wa siku hii, pamoja na jitihada zetu tunaamini kunamafanikio yatafikiwa, kuanzia ndani ya Rasimu na katiba yenyewe” alisema Hellen


Aidha Kamishna msaidizi wa wizara ya Afya na ustawi wa jamii bwana Rabikira Mushi amesema, ni wakati sasa kwa jamii nzima kutambua suala la kulinda haki za watoto ni la jamii nzima na kwamba kila halmashauri ina wajibu wa kulinda haki za watoto katika maeneo yao.

“Halmashauri zote zinatakiwa kujali watoto kwenye maeneo yao bila kujali huyu ni mzaliwa wa hapo au nimgeni kwani jukumu la watoto nilakwao kisheria na sio ombi, pamoja na jamii nayo itambue hilo sio kuwaachia serikali tu nilazima kila mtu ajiwajibishe juu ya kulinda haki za watoto” Alisema Rabikira

Miongoni mwa watoto waliohudhuria maadhimisho hayo kutoka shule mbalimbali,Blo hii ilipata fursa ya kuongea na Aneth George kutoka Kibasila Sekondari pamoja na Adnan Kaizer kutoka
Makongo Sekondari wakielezea jinsi gani wameipokea siku hiyo na mapendekezo yao kwa jamii juu ya haki za watoto


Aneth alisema, Hakizao nilazima zilindwe na kuwa Serikali iteuwe siku moja kwa watoto kujadili haki zao ndani ya Rasimu ya katiba mpya ilinao wajue hakizao zitakazo kuwepo katika kabita mpya. Alisema Aneth

Adnan Kaizer kwa upande wake amesema, suala la wazazi hasa wa kambo kuwatumikisha watoto kinyume na uwezo wao na sheria isemavyo sio haki nakuwa kila mtu awajibike kumlinda mtoto. Aslisema Adnan

Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka Duniani kote, tarehe 16 June lakini shirika la LHRC limeamua kufanya hii leo. Kimataifa shirika la Kazi Duniani ILO lilitoa ripoti yake kuhusiana na siku hiyo ambapo watoto Milioni 10.5 barani Afrika wanatumikishwa majumbani


EmoticonEmoticon