Mashirika mbalimbali yanayohusika na utetezi wa haki za binadamu
yameipongeza tume ya Katiba kwa kuweka kipaumbele katika suala la haki za
binadamu katika rasimu ya katiba mpya iliyozinduliwa hivi karibuni.
Wakizungumza na Blog hii leo jijini Dar es salaam, mratibu wa
katiba kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Anna henga pamoja na
Mratibu kutoka mtandao wa Mashirika ya haki za binadamu kusini mwa Afrika bi
Martina Kabisama, wamesema pamoja na mazuri yaliyomo kuhusu haki za binadamu,
tume ya katiba inatakiwa kuliangalia upya suala la adhabu ya kifo.
“Mtu anahaki ya kuishi, kuendelea kuwepo kwa
kifungu kinachoruhusu adhabu ya kifo kwakeli nikinyume cha haki ya kila mtu
kuishi, hivyo tunaliangalia zaidi hilo swala la adhabu ya kifo ambayo
imependekezwa kwenye rasimu hii ya sasa” Alisema Anna Henga
Wanaharakati hao pia wamesema kuwa muda wa miezi miwili uliobaki
kuelekea bunge la katiba hautoshi kwa wananchi kuielewa rasimu hiyo na hapa
wanatoa mapendekezo.
Muda uliotolewa kuchambua
rasimu hii kwa wananchi ni mdogo sana, kutokana na mambo yote kuwagusa moja kwa
moja lakini kwa sisi wanaharakati au asasi mbalimbali ni rahisi kwani utaanza
kusoma hasa kipengele kinacho kuhusu tu nakukitolea maamuzi haraka, Alisema
Anna Henga
Naye Bi. Martina Kabisama
ameongeza kuwa kutokana na wao kupewa fursa ya kutengeneza baraza la haki za
binadamu nirahisi kukaa na kujadili nini tunataka kiwepo au kushugulikiwe vipi,
ila upande wa wananchi itakuwa ngumu sana
Kituo cha Sheria na haki za binadamu kinakemea kitendo cha baadhi
ya watu kuwekea mkazo masuala ya kisiasa pekee na kuacha mambo mengine ya
msingi, Bi Anna anafunguka zaidi.
“Mpaka sasa watu wanaochambua rasimu hii wanalenga tu maswala ya
siasa na kuacha mambo ya kijamii ambayo yanawalenga zaidi watanzania, hatuguswi
na siasa tuu tujadili na mapendekezo ya Elimu, Afyana na mengine kama Afya ya
watoto, tujadili na hayo pia sio siasa tuu” alisema Anna Henga
Asasi mbalimbali za kiraia zikiwemo LHRC na SAHRINGO hivi sasa
zipo katika hatua ya kuunda mabaraza ya katiba yatakayojadili rasimu hii, kabla
ya bunge la katiba litakalopitisha rasimu ya mwisho, kuundwa Mwezi Agosti mwaka
huu.
EmoticonEmoticon