Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kimeichukuliwa hatua ya serikali ya kutangaza dau la shilingi Mil. 100 kwa yeyote atakaye fichua taarifa za kumtia hatia aliye husika na tukio la kurusha bomu lililo sababisha vifo vya watu 4 nakuacha wengine 50 wakiwa wamejeruhiwa vibaya

Hatua hiyo iliyopingwa na Chadema ilitangaza jana Bungeni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Mh. Willium Lukuvi ambapo Mkurugenzi wa habari na mawasiliano Mhe. John Mnyika amesema kitendo hicho nikutumia vibaya fedha na rasilimali za serikali

Akiongea hii leo jijini Dar es salaam katika makao makuu ya chama hicho, Mhe. Mnyika amesema fedha hizo ambazo serikali imezitangaza Ingekuwa bora kama wangezitumia kuwa fariji majeruhi na waliopoteza ndugu zao katika tukio hillo, amesema Mnyika

Mnyika amesema, chama hicho kimetoa Baraka zote kwa wabunge wake kutohudhuria Bungeni mpaka pale maombolezo yatakapo malizika huko Arusha na kwamba Mbunge yeyote wachama hicho hataruhusiwa kuhudhuria Bungeni

Aidha Mhe. Mnyika ameongeza kuwa chama hicho kimesikitishwa na kitendo cha Bunge kutositisha shuguli zake kutokana na tatizo la Arusha wakati majanga kama haya yanapotokea kwani kwa mujibu wa kanuni za Bunge inaruhusiwa kusimamisha shuguli zote mpaka hali ikae sawa.

“Bunge linatumiwa na serikali kuchamazisha haki, Polisi nao wanatumika na Serikali lakini ukweli ni kwamba bado tuna muhimili wa mahakama ambayo naamini yenyewe itasimamia haki daima”alisema Mnyika.

Kuusiana na mkanda wa video ambao chama hicho inadai inamuonyesha Polisi wa kikosi cha FFU akilipua bomu hilo, Mnyika amesema watasubiri mkanda huo kupitiwa na mwanasheria kwanza na viongozi wengine wajuu wa chama hicho iliwaweze kuitoa kwa wananchi wote kuiona

“Mkanda tunao na ushahidi hupo, tusubiri taratibu za kuupitia ilituweze kuangalia hasara na faida za kuutoa kama tutaona inafaa ama laa kila mtu hatauona mkanda huo”Alisema

Chama cha CCM na CHADEMA vimekuwa vikitupiana lawama kutokana na vifo vya watu 4 vilivyo sababishwa na kulipuka kwa bomu huko eneo la Soweto, jeshi la polisi likiwa kiwa limeunda kamati kuchunguza tukio hilo


EmoticonEmoticon