MAMIA WAMPOKEA MANGWEAR, WENGI WATAKA KUMBEBA KWA MSURURU MREFU

Mamia hivi sasa wamejikusanya kando kando ya barabara Pugu Road maeneo ya Viwanja vya ndege wakitaka kuuubeba mwili wa marehemu Mangwear uliwasili hii leo kutoka Afrika kusini.



Mwanahabari aliyopo katika eneo hilo ameiambia Blog hii kuwa mpaka sasa msafara kuelekea Hospitali ya Muhimbili unaenda kwa kasi ndogo kutokana na watu wengi kutaka kuuubeba mwili huo, wakati huo huo kamati ya mazishi yake ilikwisha andaa gari kwaajili ya kuubeba mwili huo 


Mangear atazikwa nyumbani kwao huko mkoani Morogoro, marehemu ulitarajiwa kuwasili mwishoni mwa wiki iliyopita lakini ikashindikana kutoka na sababu za kiusalama,pamoja na sababu za uchunguzi wa mwili wake uliyokuwa ukifanywa na jopo la Madaktari nchini Afrika Kusini.


EmoticonEmoticon