Mamlaka ya Elimu nchini imetoa
jumla ya madawati 420 kwa shule za msingi 12 katika wilaya ya masasi
mkoani Mtwara yenye jumla ya shilingi Millioni 79 nakuweza kupunguza
upungufu wa madawati katika wilaya hiyo
Akiongea na Blog hii katika
ofisi za mamlaka hiyo hii leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi
wa TEA bi. Sylvia Lupembe amesema madawati hayo yamepunguza upungufu
kutoka asilimia 22 hapo awali mpaka kufikia asilimia 17 hivi sasa
“Wilaya yote ya Masasi ilikuwa
na upungufu mkubwa wa madawati lakini kwakuanzia tumeanza na idadi ya
madawati 420, na hii ni awamu ya kwanza tunategemea kupeleka awamu ya
pili hukohuko Masasi” alisema Lepembe
Aidha bi Sylvia Lupembe
amewaomba wafadhili mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kusaidia
mamlaka hiyo katika mambo mbalimbali kama ujenzi wa Madarasa, vitabu
pamoja na madawati ili kuweza kuinua sekta ya Elimu nchini
“Tuchangie elimu yetu kupitia
mfuko wa Elimu ili kuweza kuboresha miradi ya elimu hapa nchini, na
tunapokea hata kwa wafadhili wa nje pia wandani na kushirikiana nao
vyema,”Alisema Lupembe
Mkoa wa mtwara ambako wilaya ya
masasi unapatikana ni miongoni mwa mikoa inayofanya vibaya katika
matokea ya kidato cha nne na shule za msingi kutokana na ukosefu wa
vitendea kazi kwa walimu, madarasa vitabu hata madawati.
EmoticonEmoticon