WANANCHI WA AFRIKA KUSINI WAENDELEA KUMWOMBEA MANDELA

    

Hali ya Raisi wa kwanza mweusi nchini Afrika kusini Nelson Madiba Mandela mwenye umri wa miaka 94, imeelezwa kuwa ni mbaya na amekata kauli huku wananchi wan chi hiyo wakiendelea kumwombea

Hapo jana Ikulu ya Afrika Kusini kupitia Rais wake bwana Jackob Zuma ili tangaza kuwa hali ya Raisi huyo mstaafu kuwa ni mbaya,  ikiwa ni mara ya kwanza kwa Raisi huyo kujitokeza hadharani nakukiri kwamba hali ya Mandela sio nzuri

Rais Jackob Zuma aliwatangazia wananchi wake kujiandaa kusherehekea sherehe ya Raisi Mandela ambayo ni mahususi kama kumuenzi ifikapo Julai 18 ambayo ni tarehe ya kuzaliwa kwa muasisi huyo.

“We must all be planning what to do next month in marking our 67 minutes of doing good for humanity as called upon by Madiba to do so, when he lauched the International Mandela Day Campaing”Zuma said Let us make it the biggest Mandela Day ever on the 18 of July on doing good all over the country


Habari zilizo chapishwa na vyombo vya habari mbalimbali  nchini humo zinasema kuwa ndugu walionekana wakiiingia Hosptalini  humo lakini bila kusema chochote, na zaidi ni kuwa Familia ya Mandela ili kaa kikao hapo jana huko Qunu eneo ambalo aliko kulia Raisi huyo lakini yaliyo zungumzwa bado ni siri ya familia yake.

Katika sherehe iliyoandaliwa na nchi hiyo ambayo itafanyika tarehe 18 Jully ambayo itakuwa mahususi kwaajili ya matendo mema kwa jamii ndani ya nchi hiyo ndio tarehe ya kuzaliwa kwa Mandela ambapo atatimiza miaka 95. 


EmoticonEmoticon