MLIPUKO ARUSHA, SERIKALI KUTOA MILIONI 100 KUMPATA MTUHUMIWA



Huku watanzania wakiwa katika hali ya sinto fahamu kutokana na bomu lililolipuka huko Arusha na kujeruhi watu zaidi ya 55 huku watu 3 wakiwa wamefariki hadi hivi sasa kutokana na Bomu hilo



Tayari Serikali imeunda tume kuchunguza tukio hilo, pamoja na kutoa kiasi cha Shulingi Millioni 100 kwa mtu yeyote atakaye toa taarifa za kumkamata mtu ambaye anahusika na tukio hilo ilihatua zaidi ziweze kuchukuliwa



Akiongea mapema leo Bungeni,Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa Bunge Mhe. William Lukuvi amesema serikali itatoa jumla ya shilingi Milioni 100 kwa yeyote atakaye mtaja aliyehusika na tukio hilo huku akiwasihi watanzania kuwa wamoja na kutokubali kutumiwa na watuwasio kuwa na mema kwa Taifa letu


EmoticonEmoticon