TUHUMA ZA RUSHWA DHIDI YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU ZILIZOTOLEWA NA CHADEMA

CHADEMA yamnasa Waziri Mulogo kwa rushwa

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemfikisha Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo, mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kutoa rushwa ya ahadi ya mifuko ya saruji na fedha taslimu 40,000 kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi.

Chama hicho pia kimemfungulia faili la tuhuma za ubakaji mgombea udiwani wa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Mbalamaziwa, Zuberi Nyomolela, kwa kosa kuishi kinyumba na binti mwanafunzi.

Hayo yamesemwa jana katika kijiji cha Mbalamaziwa na mwanasheria wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Sinkara Lucas, kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Mbalamaziwa, uliohudhuriwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe.



EmoticonEmoticon