FURSA ZA AJIRA ZATAJWA NA MTANDAO UNAO TOA AJIRA FEKI NAO WAPONDWA

Sekretariet ya Ajira nchini imeainisha fursa za ajira zilizopo serikali na kuwataka wahitimu au wanafunzi wanaopata fursa ya kujiunga na elimu ya juu kukimbilia fursa hiyo ilikutatua tatizo la ukosefu wa ajira baada ya kuhitimu

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam, Katibu Sekretariet ya Ajira bwana Xvavier David amesema fursa hizo zipo kwa wingi lakini wanafunzi wengi hupuuzia swala hilo nakujikuta katika ukosefu wa ajira

“Kuna nafasi za ajira kwenye Ualimu, Utabibu, Afisa utendaji, Kilimo ambazo wahitimu wake sio wengi na nafasi za Ajira zipo nyingi hivyo niwatake wahitimu kukimbilia huko nasiokuwa wote tutakumbilia taaluma zilezile baadae ajira zina kosekana”Alisemai ikiwemo mitandao ya kijamii

Aidha, Xvavier David amekanusha vikali taarifa zinazotolewa na mtandao wa www.eastafricajobscareer.com lenya tangazo zinalosema KAZI UTUMISHI JULAI 2013, pamoja na KAZI UTUMISHI AUGUST 2031 JOB IN TANZANIA" kuwa sio ya kweli na kwamba huo ni upotoshaji

"Huu ni upotoshaji mkubwa kwa kuwa matangazo hayo yanasababisha usumbufu mkubwa kwa umma, na tumekuwa tukisumbuliwa mara kwa mara wakati sekretariet  ya Ajira haijatoa matangazo haya na tovuti hiyo inafanya hivyo kwaajili ya kujipatia fedha hivyo wajihadhari na matapeli hao" alisema Xvavier

Tungeomba watembelee tovuti yetu ya www.ajira.go.tz ambayo inamatangazo yetu au wapige simu no. 255 - 687624975 ili kupata habari na taarifa sahihi za ajira hapa nchini, na kuwa wanafanya mchakato wa kuwatambua wamiliki wa tovuti hiyo ili waweze kuongea nao juu ya swala hilo. Alisema Xvavier

Naomba kufahamisha umma kuwa sekretariet ya Ajira aiwajibiki nawala haitawajibika kwa taarifa ama matangazo yanayohusu Ajira Serikalini katika vyombo mbalimbali vya habari, hivyo nawataka wote wanaoendelea kutoa matangazo hayo ua uongo/kughushi yenye lengo la kupotosha umma kuacha maramoja. Alisema Xvavier

Hatahivyo, Xvavier amewaomba wale wote walioomba ajira katika usaili wa tangazo la kazi lililotolewa tarehe 26 Machi, 2013 kuwa wale wote ambao wamekidhi zigezo vya Ajira yatatolewa katika mtandao wa sekretariet ya Ajira wiki ya kwanza ya mwezi Julai 2013 hivyo kuwataka kutembelea mtandao wa ajira kupata tarifa zaidi

Xvavier amesema kuwa wanaoomba kazi serikalini watambue kuwa fursa za Ajira ni za ushindani nakuwa sasa hivi watu niwengi na serikali inahitaji watumishi wenye uwezo wa kitaaluma na kiutendaji ili kuweza kuwahudumia watanzania. 


EmoticonEmoticon