TETESI ZA KUIBUKA VURUGU MTWARA, MADUKA YAFUNGWA TENA LEO

Tetesi yakuwa huenda kutakuwa na vurugu mkoani Mtwara, baada ya Mbunge wa Mtwara mjini Mhe. Hasnein Murji kukamatwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma zinazosemekana kuwa ni kuchochea wakazi wa eneo hilo kutofungua maduka yao au kutofanya shuguli za kijamii ili waweze kujitokeza mahakamani kusikiliza kesi za wale waliokamatwa hapo awali baada ya kuzuka Vurugu

Majira ya asubuhi hali ilikuwa kama uonavyo pichani huko mkoani mtwara, maduka mengi yamefungwa lakini Habari zaidi zilizoifikia Blog hii zinasema baadhi ya magenege walionekana watu wengi wakinunua vitu kwa wingi endapo vurugu zikijitokeza waweze kuwa na chakula cha kutosha

Picha imepigwa na Revocatus - Mtwara
Hapo jana ili ripotiwa kuwa baadhi ya wakazi waeneo hilo walianza kuyakimbia makazi yao kwa kuhofia kutokea kwa vurugu zingine kama za kipindi cha mwezi jana ambapo zilizuka vurugu kubwa katika mji wa Mtwara na viunga vyake baada ya wananchi wa mji huo kuandamana baada ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa .

Picha imepigwa na Revocatus - Mtwara
Madai ya wakazi wa Mtwara ni kutotaka Bomba la kesi ku safirishwa kuja Dar, lakini  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo ameendelea kusisitiza kuwa msimamo wa serikali juu ya mpango wa kusafirisha Gesi hiyo uko palepale


EmoticonEmoticon